title : STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS
kiungo : STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS
STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS
MCHEZAJI maarufu wa zamani wa Timu ya Arsenal ya Uingereza Robert
Pires amewasili nchini Tanzania leo Novemba 1,2018 kwa mwaliko maalum wa Benki ya Barclays kwa lengo la kushiriki uzinduzi wa Kampeni ya benki hiyo inayoitwa Superfans.
Pires akiwa nchini kwenye kampeni hiyo ambayo itampa nafasi mteja mwenye akaunti ya biashara au anayetumia kadi kufanya manunuzi mara nyingi kipindi cha kampeni fursa ya kujishindia bahati nasibu ya safari ya Uingereza kushuhudia mechi moja mubashara ya ligi Kuu ya Uingereza.
Akizungumza leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya Pires kutua nchini, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania Aron Luhanga amesema ujio wa mchezaji huo ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni hiyo na atakuwa nchini kwa siku tatu.
"Gwiji wa zamani wa timu ya Arsenal Robert Pires amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuzindua kampeni ya wateja iitwayo Superfans inayomwezesha mteja anayemiliki akaunti ya biashara au anayetumia kadi ya Barclays kufanya manunuzi mara nyingi kuzawadiwa safari ya Uingereza kushuhudia mechi mubashara ya Ligi Kuu ya Uingereza,"amesema.
Hivyo makala STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS
yaani makala yote STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/staa-wa-zamani-wa-arsenal-robert-pires.html
0 Response to "STAA WA ZAMANI WA ARSENAL ROBERT PIRES AWASILI NCHINI KWA MUALIKO WA BARCLAYS"
Post a Comment