title : MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI
kiungo : MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI
MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Dodoma
MBUNGE wa Lilwale kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)Zuberi Kuchauka amesema huu sasa ni muda wa kufanya kazi na kutekeleza Ilani ya Chama hicho kwa kasi ya Rais Dk.John Magufuli katika jimbo lake.
Kuchauka amesema hayo Mjini Dodoma ambapo anashiriki Bunge la 11 ,kikao cha 13 mara baada ya kuapishwa kuwa Mbunge kwa tiketi ya CCM.
"Nawashukuru wananchi wa Liwale kwa kuendelea kuniamini katika kipindi kingine nikiwa ndani ya CCM.Mnakumbuka nilikuwa upinzani na kisha kujiunga CCM na leo ni mbunge kupitia chama hicho.Nawashukuru wananchi kwa kuendelea kuniamini.
" Niwahaidi wakazi wa Liwale kuwa sitowaangusha katika miaka miwili iliyobaki.Nitashirikiana nanyi katika kuhakikisha jumbo letu linapata maendeleo kwa kasi,"amesema Kuchauka
Amesema kuwa katika miaka hii miwili ambayo imebaki atahakikisha anaendeleza pale alipoishia kwani uwanja ni ule ule na kilichobadilika ni timu ambayo amejiunga nayo ambayo ni sahihi kwa kuleta maendeleo ya Jimbo la Liwale.
Amefafanua yeye ni Mbunge wa CCM na Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM chini ya Rais Dk. Magufuli ambaye msimamo wake ni kusaidia watu maskini na kuchapa kazi kwa bidii.
Pia ameshukuru viongozi wa CCM pamoja na wananchi wote kwa kumuamini na kurudi kugombea tena katika uchaguzi Mdogo na hatimaye kuibuka na ushindi.
MBUNGE wa Lilwale kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Zuberi Kuchauka alipofanya mahojiano mafupi na Michuzi TV jijini Dodoma.
Hivyo makala MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI
yaani makala yote MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mbunge-wa-liwale-asema-huu-sasa-ni-muda.html
0 Response to "MBUNGE WA LIWALE ASEMA HUU SASA NI MUDA WA KUFANYA KAZI,AWASHUKURU WANANCHI"
Post a Comment