title : Mawaziri Watakiwa Kufanya Maamuzi.
kiungo : Mawaziri Watakiwa Kufanya Maamuzi.
Mawaziri Watakiwa Kufanya Maamuzi.

Na. Mwandishi Wetu-MAELEZO
Rais Magufuli amewataka Mawaziri kufanya maamuzi ya haraka na yenye tija katika mambo yanayohusu wizara zao ili kuongeza ufanisi na kuchochea juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Ikulu, Jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuwaapisha Mawaziri wawili, Manaibu Waziri wanne na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria aliowateua hivi karibuni.
Akizungumza katika hafla hiyo Rais Magufuli alibainisha kuwa Mawaziri wanapaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na kutoa maamuzi sahihi bila ya kusubiri maelekezo kutoka kwake au kwa Waziri Mkuu.
“Mawaziri muwe mnafanya maamuzi kwenye mambo yaliyomo kwenu, sio kila kitu mpaka Waziri Mkuu au Rais afanye, mimi nawapenda mawaziri wanaofanya maamuzi,” alisisitiza Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli aliwataka mawaziri kuridhika na baadhi yao waache kutumia ndugu au watu wengine kuwadhulumu wakulima wa korosho kwa kufanya biashara ya ‘kangomba’.
Pia aliwasisitiza wateule hao wapya aliowaapisha leo, kuanza kazi mara moja kwa kushirikiana ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amezitaka bodi za mazao zijitathmini na Serikali itakagua utendaji kazi wa kila bodi ili kuhakikisha zinafanya kazi kwa maslahi ya wakulima.
Sambamba na hayo Rais Magufuli alisema kuwa Serikali itanunua korosho zote kutoka kwa wakulima kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo moja na kumtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuacha kupokea maombi ya wanunuzi binafsi wa zao hilo waliojitokeza hivi karibuni baada ya Serikali kuwataka wafanye hivyo.
“Korosho yetu ni first class kwenye soko la dunia, TADB chukueni pesa mkanunue korosho kwa bei ya sh. 3,300 wakalipwe wakulima kwa kila kilo ambayo haijabanguliwa, hatuwezi kuendelea kuwadhulumu wakulima,” alisema Rais Magufuli.
Pia aliwaagiza Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuanza kazi mara moja ya kusomba korosho na kuzipeleka kwenye maghala makubwa na wasimamie zisiingizwe korosho mbaya kutoka maeneo mengine.
Vilevile Rais Magufuli alisema kuwa kuanzia sasa kiwanda cha kubangua korosho cha BUCO kilichopo mkoani Lindi kitamilikiwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mpaka itakavyoamuliwa vinginevyo.
“Miaka ijayo tutaleta tutaleta vifaa vingine vya kisasa zaidi ili tuwe na viwanda vikubwa vyenye uwezo wa kubangua korosho nyingi hata tani laki 2,” alisema Rais Magufuli.
Kwa upande wake Spika wa Bunge, Job Ndugai alitoa rai kwa watendaji wa Wizara ya Kilimo kujipanga upya na kufanya kazi kwa weledi na ufanisi kwani wizara hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa hasa kipindi hiki kuelekea uchumi wa viwanda.
Hivyo makala Mawaziri Watakiwa Kufanya Maamuzi.
yaani makala yote Mawaziri Watakiwa Kufanya Maamuzi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mawaziri Watakiwa Kufanya Maamuzi. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/mawaziri-watakiwa-kufanya-maamuzi.html
0 Response to "Mawaziri Watakiwa Kufanya Maamuzi."
Post a Comment