title : KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU
kiungo : KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU
KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU
Kaimu Katibu Msaidizi wa timu ya mpira wa miguu Manispaa ya Kinondoni (KMC) Walter Harrison akizungumza na wadau pamoja na wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu kufukuzwa kwa mchezaji wao Abdulhalim humud
Na Khadija Seif,Globu ya jamii
Uongozi wa Klabu ya Kinondoni municipal council (KMC) umeweka wazi msimamo wao wa kumfukuza rasmi aliyekua mchezaji wao, Abdulhalim Humud. Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es salaam leo, Kaimu Katibu Msaidizi wa timu hiyo, Walter Harrison amesema mchezaji huyo amefukuzwa rasmi kutokana na utovu wa nidhamu kwa viongozi wake pamoja na wachezaji wenzake.
Harrison ameeleza kuwa, vitendo vya Humud vya utovu wa nidhamu vimekua vikijirudia mara kwa mara na kwa uongozi kushindwa kuweza kuvikabili na kulazimika kumfukuza rasmi.
"Vitendo vya utovu wa nidhamu vimekuwa vinajirudia mara kwa mara, kwa viongozi na hata wachezaji wenzake na imepelekea kushindwa kuvumulia na kulazimika kuachana nae rasmi,"amesema Harrison
Alikadhalika Humud alishawahi kuandika barua kwa uongozi wa KMC kuomba kuachwa ili asiendelee kuichezea timu hiyo kwa sasa na hivyo uongozi wakaamua alipe gharama kiasi kutokana na pesa nyingi zilitumika kama vile gharama za matibabu, mshahara pamoja na fedha zilizokua zikitumika wakati yuko kambini.
Aidha , Kaimu Katibu huyo amekumbusha wadau na wanamichezo kuwa tabia hiyo kwa Humud imekua kama ni desturi yake kwani alishawahi kufanya vitendo hivyo kwa baadhi ya timu kongwe hapa nchini.
Hivyo makala KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU
yaani makala yote KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/kmc-wamtupia-virago-abdulhalim-humud.html
0 Response to "KMC WAMTUPIA VIRAGO ABDULHALIM HUMUD KWA UTOVU WA NIDHAMU"
Post a Comment