title : Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu
kiungo : Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu
Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Phillip Mpango amesema Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu nchini Tanzania ya Mwaka 2017 (THDR) inayozungumzia “Sera ya Kijamii Katika Muktadha wa Mageuzi ya Kiuchumi”, ina mchango mkubwa katika kuchambua masuala yanayohusu maendeleo ya binadamu na nafasi yake katika uandaaji wa mipango ya maendeleo, utengenezaji wa bajeti, ufuatiliaji na tathmini.
Alisema hayo katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu wakati wa uzinduzi wa ripoiti hiyo mjini Dodoma jana.“Kwa mtazamo wangu, dhana hii ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi sio tu kwamba ni dhana sahihi bali pia inaendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2016/17 – 2020/21.’ Alisema Dk. Mpango .
Aidha, alisema dhana ya kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya kiuchumi ni dhana ambayo imekuwa ikizingatiwa katika mipango ya ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka mmoja mmoja pamoja na miongozo ya uandaaji wa bajeti za serikali.
Dk. Mpango alisisitiza kwamba kwa kuzingatia umuhimu wa kujenga uchumi jumuishi, kutokuacha mtu yeyote nyuma katika mchakato wa maendeleo na kufungamanisha maendeleo ya watu na mageuzi ya uchumi, serikali ya Tanzania imetoa umuhimu mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii ili kuinua hali za watu wake.Waziri Mpango alisema kwamba sekta ya afya, elimu na miradi ya kimkakati kama ujenzi wa reli ya kisasa ni sehemu ya juhudi zinazofanya kuwezesha uchumi jumuishi.
Mshehereshaji George Mulamula (kushoto) wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 akiitambulisha meza kuu wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly, Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo Dkt. Phillip Mpango wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa mgeni rasmi na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Bouckly ambao ni wafadhili wa ripoti hiyo akitoa salamu za Umoja wa Mataifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya Tanzania (THDR) ya mwaka 2017 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Kambarage kwenye jengo la Treasury Square mjini Dodoma. Kulia ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa ESRF, Prof. Sylvia Temu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Hivyo makala Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu
yaani makala yote Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dk-mpango-afagilia-ripoti-ya-maendeleo_29.html
0 Response to "Dk Mpango afagilia ripoti ya maendeleo ya binadamu"
Post a Comment