title : WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO
kiungo : WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO
WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO
Na Frankius Cleophace Mara
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto. Ummy Mwalimu amemuagiza katibu mkuu wa afya kuhakikisha kila Hospital za Rufaaa za Mikoa yote Tanzania kuwa na vifaa tiba vya kinywa na meno kabla ya machi 30, 2019.
Kauli hiyo imetolewa wakati akifungua mkutano wa madaktari bingwa wa kinywa na meno Tanzania katika ukumbumbi wa mwekezaji wa mkuu wa mkoa wa Mara. Waziri ummy amesema kuwa kufanya hivyo nikuhakikisha wanaondoa changamoto katika hospitali zote nakuowaondolea wananchi usumbufu wanaoupatapa kipindi wakitembea zaidi ya kilomita 200 kuitafuta huduma ya kinywa na meno.
Pia amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inawahudumia na kuwajali wananchi wote nakuhakikisha wanapata huduma zote katika maeneo yaliyokaribu nao ambapo amewakikishia Madaktari bingwa kuanzia hospital za wilaya katika mkutano ujao itakuwa tayari wameshatekeleza adhima hiyo. Naye mkuu wa Mkoa wa Mara Adamu Malima amewapongeza madkatari Bingwa wa kinywa na meno kwa kuupa kipaumbele Mkoa wa Mara katika utaoji wa huduma hiyo huku akimuomba waziri kuangalia namna ya kusaidia wananchi wa mkoa huo katika utoaji wa huduma hiyo.
Awali akitoa Taarifa mbele ya waziri wa Afya Rais wa madaktri wa kinywa na meno Ambege Mwakatobe amesema kuwa pamoja na jitihada zao zote wanakwamishwa na changamoto ya upungufu wa watalamu wa kinywa na meno ambapo baadhi ya maeneo Nchini Tanzania yanakosa upatikanaji wa huduma hiyo pia hakuna chuo ambacho kinafundisha wahudumu hao wa kinywa na meno. Zoezi la kuendelea kutoa huduma ya tiba ya kinywa na meno kwa baadhi ya Maeneo katika wilaya za Mkoa wa Mara zinaendelea ili kuweza kuwanusuru wagonjwa wa Meno.
Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza na madaktari katika mkutano wa madaktari bingwa wa kinywa na Meno uliofanyika katika ukumbi wa Mwekezaji Mkani Mara.
Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima akiongea na madaktari hao katikati ni Waziri wa Afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu na wakwanza kulia ni Rais wa madaktri wa kinywa na meno Ambege Mwakatobe.
Rais wa madaktri wa kinywa na meno Ambege Mwakatobe akizungumza katika mkutano huo.
Daktari Merina Njelekela ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi akiongea katika Mkutano huo wa madakri bingwa wa kinywa na Meno uliofanyika mkoani Mara.
Hivyo makala WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO
yaani makala yote WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/waziri-wa-afya-ummy-atoa-maagizo.html
0 Response to "WAZIRI WA AFYA UMMY ATOA MAAGIZO UPATIKANAJI WA VIFAA TIBA ZA KINYWA NA MENO"
Post a Comment