DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI

DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI
kiungo : DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI

soma pia


DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) imefanikwia kuunganisha wateja wapya 2881 katika mfumo mpya wa ugawaji maji ambao umekamilika kujengwa kwenye miradi tofauti ya Mamlaka hiyo.

Kazi hiyo iliyoanza Oktoba Mosi mwaka huu imeweza kufanikisha kuunganisha wateja wapya na inaendelea kwa kasi kwenye maeneo tofauti ya Mkoa wa Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani.

Akielezea maunganisho hayo mapya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Jamii DAWASA Neli Msuya amesema kuwa mpaka sasa maunganisho mapya yanaendelea kwa kasi katika maeneo ya Salasala, Kilimahewa na Kinzudi, Kiluvya, Kiluvya madukani, Gogono, Hondoro na Kiamba pamoja na  Bagamoyo- Kiembeni.Amesema, lengo ni kuunganisha wateja wapya 60,000 (Elfu Sitini) katika eneo la Salasala na wateja 100,000 (laki moja) katika eneo lilipo kati ya Kiluvya na Mbezi.

"Wateja wapya 2881 wameshaunganishwa maeneo yaliyopo, idadi ikiwa 1624 kwa Salasala- Kinzudi, Kiluvya- Mbezi 1111 na Bagamoyo 146 hivyo bado kunwa uwezekano wa wateja wengi zaidi kuendelea kuunganishwa,"amesema.

Amesema Katika kuhakikisha kuwa maji yalioongezeka yanawafikia wananchi wengi zaidi hasa katika maeneo ambayo zamani hayakuwa na mtandao wa mabomba, miradi mikubwa na midogo imetekelezwa ikiwemo uoanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini kukiwa na  ujenzi wa matenki ya maji matano yenye ujazo wa kati ya lita milioni 5.0 na 6.0 pamoja na ulazaji wa mtandao wa mabomba.

Msuya amesema, maeneo hayo yote yanapata maji kutoka katika mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini na ili kuharakisha kazi ya uunganishwaji wa majisafi kwa wananchi wote, wananchi wanakumbushwa kuwa uunganishwaji mpya unatolewa kwa Mkopo.Aidha, ameeleza kuwa DAWASA itagharamia vifaa, uchimbaji wa mtaro na mabomba ya maji yataunganishwa katika malipo ambayo mteja atarerejesha ndani ya muda wa miezi sita.

Matenki hayo  yamejengwa katika maeneo ya Changanyikeni, Salasala,Wazo, Mabwepande na Bagamoyo na katika maeneo yote ya miinuko ili kuwezesha maji kufika katika maeneo mengi Zaidi kwa msukumo mzuri na mradi huo umetekelezwa na serikali kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka benki ya Exim ya India.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo akitoa pongezi kwa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) kwa kufanikisha uunganishwaji wa Wateja wapya 2881 katika mfumo mpya wa ugawaji maji ambao umekamilika kujengwa kwenye miradi tofauti ya Mamlaka hiyo.


Hivyo makala DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI

yaani makala yote DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/dawasa-yaunganisha-wateja-wapya-2881.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DAWASA YAUNGANISHA WATEJA WAPYA 2881 KATIKA MFUMO MPYA WA UGAWAJI MAJI"

Post a Comment