21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE

21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa 21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : 21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE
kiungo : 21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE

soma pia


21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE

Na Mwandishi wetu Tunduru

MAHAKAMA ya Mwanzo Mbesa wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma,imewahukumu kifungo cha miezi mitatu jela au kulipa faini ya shilingi laki tatu wazazi 21 baada ya kupatikana na kosa la kushindwa kupeleka watoto wao shule.

Aidha, mahakama hiyo imetoa hukumu ya kuchapwa viboko vinne kila mmoja watoto 21 ambao ni wanafunzi wa shule ya sekondari Mbesa kwa kosa la kutokwenda shule.

Hukumu hiyo imetolewa jana na hakimu wa mahakama ya Mwanzo Mbesa Kavula Katabu ambapo wazazi wawili kati yao,waliachiwa huru baada ya kulipa faini.Akitoa hukumu hiyo mbele ya mamia ya wananchi wa kijiji cha Mbesa waliofika mahakamani hapo hakimu Katabu alisema,wazazi hao wametiwa hatiani kwa mujibu wa kifungu cha 8(E) na kifungu cha 14 cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009.

Kwa upande wa wanafunzi Katabu alisema, wamekutwa na kosa la kukataa kwenda shule na hivyo kuwatia hatiani wanafunzi hao kwa mujibu wa sheria ya Elimu namba 25 cha mwaka 1978 kifungu cha 2 na kifungu kidogo cha 4.

Wakizungumza nje ya mahakama,baadhi ya wananchi wamepongeza uamuzi wa mahakama kwa kutoa hukumu hiyo kwa kuwa itasaidia sana kupunguza tatizo la utoro kwa wanafunzi na wazazi wenye tabia ya kukatisha masomo watoto wao na badala yake wanawafanyisha kazi za nyumbani ikiwemo kuokota korosho mashambani.

Ali Mohamed na Rashid Said walisema, hukumu hiyo imefika kwa wakati muafaka kwani ndiyo msimu wa kuandikisha watoto wenye sifa ya kuanza elimu ya awali,msingi na wale watakaochaguliwa kuingia kidato cha kwanza.Kwa upande wake,mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera alisema, operesheni ya kuwasaka wazazi na watoto wasiotaka kwenda shule ni endelevu katika tarafa zote saba katika wilaya hiyo.

Amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanapeleka watoto wao shule kupata elimu ambao ndiyo urithi mkubwa kwa mtoto badala ya kuanza kuwafanyisha kazi za nyumbani ambazo zina changia sana tatizo la umaskini kwa baadhi ya kaya.


Hivyo makala 21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE

yaani makala yote 21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala 21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/21-jela-kwa-kushindwa-kuwapeleka-watoto.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "21 JELA KWA KUSHINDWA KUWAPELEKA WATOTO WAO SHULE"

Post a Comment