title : WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO
kiungo : WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO
WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO
Na Tiganya Vincent
MKUU wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla amewataka wazazi Mkoani Tabora kutowazuia watoto wao kushiriki katika shughuli mbalimbali za elimu ya kujtegemea kama vile ufugaji na utunzaji wa mifugo ya shughuli na kulima mashamba ya shule yao ili ziweze kuwajengea ujuzi utakaowasaidia baadaye.
Alisema elimu ya kujitegemea inamwezesha mwanafunzi hata kabla au baada ya kumaliza elimu yake ya Msingi kuwa na ujuzi wa kufanya shughuli mbalimbali kitalaamu ikiwemo kuachana kilimo au ufugaji wa kizamani ambacho hakina tija.
Makalla alitoa kauli hiyowilayani Uyui mkoani Tabora wakati wa ziara ya viongozi wa Mkoa wa Katavi kujifunza juu ya uendeshaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania ambao wanatarajia kuanza kuutekeleza katika eneo lao.
Alisema elimu ya kujitegemea itawasaidia watoto kutoa ujuzi walioupata shuleni na kuupeleka ujuzi huo kwa wazazi wao na hivyo kuwa na uzalishaji wa mifugo na mazao ya kilimo kwa tija.
“Mtoto akielimishwa juu ya upandaji kwa kuzingatia vipimo na mistari tangu shule atasaidia kuambukiza elimu hiyo kwa wazazi wake na hivyo kuwa na uzalishaji wa bidhaa nyingi kwa matumizi yao na viwanda vyetu” alisema.
Makalla alisema wazazi wakiona watoto wao wanafundishwa elimu ya kujitegemea kama vile ufugaji , kilimo cha kisasa, wasione kama ni adhabu bali ni faida kubwa wanayopatiwa watoto wao na jamii kwa ujumla.
Aidha Mkuu huyo wa Katavi na ujumbe wake umefurahishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kuinua elimu na kuongeza kipato katika shule mbalimbali mkoani Tabora chini ya Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania.
Alisema kwa kutumia Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP –Tanzania Halmashauri kama ile ya Wilaya ya Tabora -Uyui imefanikiwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika Shule ya Msingi ILolangulu kwa kiasi cha shilingi milioni 35.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla (mwenye miwani) akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Uyui mara baada ya kutembelea mradi wa ufugaji kuku chini ya Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP wakati walipotembelea Mkoa wa Tabora kwa ajili ya kujifunza.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla (mwenye miwani) akiwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui) Said Ntahondi (kulia) wakiwa kwenye moja wa madarasa wakati alipoongoza ujumbe kutoka Mkoa wake kuja Tabora kujifunza utekelezaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP.
Afisa Taaluma Mkoa wa Tabora (RAO) Silvano Sichone akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP kwa ujumbe wa Mkoa wa Katavi walipofika Mkoani humo kwa ajili ya kujifunza mafanikio yaliyotokana na mpango huo.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Amos Makalla miwani) alizungumza na walimu wa Shule ya Msingi Majengo(hawapo katika picha) wakati alipotembelea Mkoa wa Tabora kujifunza jinsi ya utekelezaji wa Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Tanzania – EQUIP. Picha na Tiganya Vincent
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO
yaani makala yote WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wazazi-wahimiza-kuunga-mkono-elimu-ya.html
0 Response to "WAZAZI WAHIMIZA KUUNGA MKONO ELIMU YA KUJITEGEMEA KWA WATOTO WAO"
Post a Comment