title : DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata
kiungo : DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata
DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata
Na Heri Shaban
MKUU wa Wilaya ya Ilala Dar es Salaam Sophia Mjema ameagiza Baraza la Hafidhi ya Mazingira (NEMC) kivunja nyumba zilizopo mpaka wa Ubungo na Wilaya ya Ilala mto Tenge.
Tamko hilo lilitolewa Dar es Salaam jana wakati wa ziara yake wilayani Ilala iliyolenga kutatatua kero za wananchi wilayani humo .Akitoa agizo hilo kwa Mratibu wa Mazingira Kanda Mashariki( NEMC) Jaffar Chingaga Mjema alilitaka Baraza hilo kutekeleza agizo la uvunjaji nyumba zote zilizofanya uharibifu eneo la mto Tenge
"Naagiza ofisini yako ya NEMC ije ivunje nyumba hizi ili upanuzi wa mto uweze kufanyika nyumba zote ziache mita 60 kwa ajili ya hifadhi mto wa bonde la mto Tenge "amesema Mjema. Amesema mara baada kuvunjwa kwa nyumba hizo atawasiliana na Mkuu wa wilaya ya Ubungo waweze kumchukulia hatua watendaji wa Manispaa yake wakiotoa kibali cha eneo la hifadhi ya bonde la mto huo .
Amesema ifikie wakati kila mtu afuate sheria na ajue kwamba Serikali ipo sio kila kitu kuvunja sheria hivyo katika hili sheria itafuatwa. Aidha amesema hivi karibuni katika Wilaya ya Ilala zoezi la urasilimishaji makazi linatarajia kuanza, hivyo washirikiane wote na kutenga maeno ya huduma za jamii ili yawepo.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi Manispaa ya Ilala Paulo Mbembelwa amesema mtu yoyote katika eneo lake anayo mamlaka ya kujenga lakini kabla kujenga lazima afute kibali Halmashauri ardhi mali ya Serikali. Mbembelwa amewataka watendaji na wenyeviti wa Serikali ya mtaa kushirikiana wote kulinda mipaka ya wananchi wao kwani ni moja ya jukumu la kazi yao.
Naye mwananchi Fadhiri Msangi ameomba Serikali kuchukua hatua za haraka ili kupanua mto huo ili wasikumbwe tena na mafuriko na waliohusika wachukuliwe hatua. "Zamani katika Mtaa huu magari yalikuwa yanapita kwa sasa shida iliyopo tunashindwa kupita hata njia ya zarula wajawazito wakiumwa au yakitokea matukio ya uharifu kutokana na mto kuhamia Wilaya ya Ilala, kutoka wilaya ya Ubungo "alisema Msangi.
Mkuu wa wilaya ya Ilala SOPHIA MJEMA akiwa katika ziara yake ya kutatua kero za wananchi wa Kata ya TABATA Dar es Salam Leo kuhusiana na mpaka wa Wilaya ya Ilala na Ubungo,pichani eneo la Mto Tenge Kata ya TABATA (Picha na Heri Shaban)
Hivyo makala DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata
yaani makala yote DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/07/dc-ilala-agiza-nemc-kuvunja-nyumba_24.html
0 Response to "DC Ilala agiza NEMC kuvunja nyumba Tabata"
Post a Comment