title : WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA
kiungo : WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA
WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA
Na. Vero Ignatus , Liwale-Lindi
Wananchi wa Liwale na viunga vyake wamejitokeza kwa wingi asubuhi ya leo katika vituo vya kupigia kura kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge 2018 mkoa wa Lindi.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Liwale Luiza Mlelwa amesema jumla ya wapiga kura waliojiandikisha 55777 na vituo vya kupigia kura 158 wote hawa watapiga kura kumchagua mbunge wao pamoja na diwani kata ya Kibutuka
Balozi Ramadhani Mapuri mjumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi amesema kuwa ameshuhudia ufunguzi wa vituo, ambapo wapiga kura wamejitokeza kwa wingi na zoezi limeanza kwa wakati hivyo wananchi wasisite kwenda kupiga kura kwani uchaguzi unaendeshwa kwa Amani na Utulivu
Amesema katika vituo vya kupigia kura vya Likongowele Galani pamoja na Kituo cha Ujenzi hali ya uchaguzi ni shwari na wananchi wameendelea kujitokeza kwa wingi kupiga kura.
Wananchi hao wanapiga kura kuwachagua viongozi wanaowapenda kutoka vyama mbalimbali vya siasa, Abduli Kombo Ngakolwa kutoka chama cha wakulima AAFP, Hamis Mohamed Lihindi kutoka ACT Wazalendo, Kachauka Zuberi Mohamed (CCM) Mtesa Mohamed Rashid (CUF) na Mwajuma Noty Mirambo (UMD).
Balozi Ramadhani Mapuri mjumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi akiwa katika Kitio cha kupigia kura cha Ujenzi. Picha na Vero Ignatus.
Pichani ni foleni ya kupiga kura katika kituo cha Likongowele Galani leo asubuhi Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi. Picha na Vero Ignatus.
Mmoja ya mwananchi kama anavyooneka tayari ameshapiga kura leo asubuhi. Picha na Vero Ignatus.
Upigani kura ukiendelea kama inavyoonekana Pichani wananchi wakiwa kwenye foleni. Picha na Vero Ignatus
Wananchi wakiwa katika kituo cha kupigia kura Likongowele ghalani katika Jimbo la Liwale Mkoani Lindi leo asubuhi 13 Octoba 2018, Picha na Vero Ignatus.
Hapa ni kituo cha kupiga kura cha Ujenzi wananchi wakiwa kwenye foleni tayari kwa kupiga kura leo asubuhi. Picha na Vero Ignatus.
Hivyo makala WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA
yaani makala yote WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/wananchi-wa-jimbo-la-liwale-wajitokeza.html
0 Response to "WANANCHI WA JIMBO LA LIWALE WAJITOKEZA KWA WINGI KUTIMIZA HAKI YAO YA KIMSINGI YA KUPIGA KURA"
Post a Comment