title : MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA
kiungo : MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA
MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA

Mbali na uamuzi huo mahakama hiyo imemwamuru binti huyo amlipe fidia ya kiasi cha sh,5 milioni mkazi huyo ambaye alikuwa msaidizi wa karibu na baba yake ambaye kwa sasa anakabiliwa na matatizo ya kiafya.
Uamuzi huo ulitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Jaji Moses Mzuna katika shauri la ardhi nambari 94 ya mwaka 2016 lililofunguliwa na Fosbrook dhidi ya Isangu huku akisimamiwa na wakili John Lundu.
Katika shauri hilo Fosbrooke aliiomba mahakama hiyo imkabidhi nyumba anayoishi Isangu iliyopo mkabala na hoteli ya Duluti kwa madai ni mali halali ya baba yake mzazi ambaye ni marehemu kwa sasa na kwamba yeye ndiye msimamizi wa mirathi ya baba yake.
Akitangaza hukumu ya kesi hiyo mbele ya pande zote Jaji Mzuna alisema kwamba mahakama imejiridhisha pasi na shaka kwamba nyumba hiyo ni mali halali ya marehemu Fosbrooke na hivyo Isangu anapaswa kuondoka pindi akishajengewa makazi mapya.
Hatahivyo,Jaji Mzuna aliieleza mahakama hiyo kwamba Isangu anapaswa kukabidhi ardhi,nyumba na samani zilizopo ndani ya nyumba hiyo na kushindwa kutii agizo hilo atastahili kulipa kiasi cha sh,500,00 kwa mwezi hadi pale atakapoondoka katika nyumba hiyo.
Katika hukumu hiyo Jaji Mzuna alisema kwamba upande wa mdaiwa utalazimika kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi huku akisisitiza kwamba wadaiwa wana haki ya kukata rufaa endapo hawajaridhika na hukumu hiyo.
Akizungumza mara baada ya hukumu hiyo wakili wa mdaiwa,Neema Osca alisema kwamba mteja wake hajaridhika na hukumu ya kesi hiyo na hivyo wanajipanga kukata rufaa kama mahakama ilivyoagiza.
Hatahivyo,Hemed Isangu ambaye ni mtoto wa Juma Isangu alisema kwamba wao hawajaridhika kabisa na hukumu ya kesi hiyo kwa kuwa wosia wa marehemu Fosbrooke ulieleza bayana kwamba endapo baba yake akitaka kuondoka katika nyumba hiyo basi awasilishe gharama kwa familia na wainunue kwa gharama inayostahiki.
“Hatujaridhika kabisa na hukumu ya hii kesi kwa kuwa hii nyumba baba yangu alipewa na marehemu Fosbrooke kama fidia ya kiinua mgongo baada ya kufanya kazi kama msaidizi wake kwa muda mrefu”alisema Isangu
Hivyo makala MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA
yaani makala yote MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/04/mahakama-yaamuru-aliyekuwa-msaidizi-wa.html
0 Response to "MAHAKAMA YAAMURU ALIYEKUWA MSAIDIZI WA DC AJENGEWE NYUMBA"
Post a Comment