Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya

Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya
kiungo : Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya

soma pia


Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Dkt. Doroth Gwajima akiangalia mtoto ambaye amezaliwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya Kitengo cha Wazazi Meta. Baadhi ya wajumbe wa Bodi na Maofisa wa NHIF walitembelea hospitali hiyo kuangalia huduma za wanazopata wanachama wake.

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

Katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Uongozi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umetembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya na baadhi ya Vituo mkoani humo kwa lengo la kuangalia huduma wanazopata wanachama wake.

Katika ziara hiyo, ujumbe wa NHIF ulikutana na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Kitengo cha Wazazi Meta na Hospitali ya Uyole ambapo pamoja na mambo mengine walijadili juu ya huduma zinazotolewa kwa wanachama wa Mfuko.

Akiongoza ziara hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Bwana Tryphon Rutazamba alisema kuwa mbali na kujadili huduma lakini pia wamepata fursa ya kukagua mradi wa Jengo la Wodi ya Daraja la Kwanza inayojengwa pamoja na uzalishaji wa Maji tiba katika hospitali ya Rufaa Mbeya kwa fedha za Mkopo wa NHIF.

“Tumepita na kuangalia maeneo ambayo wanachama wetu wanapata huduma, tumeona pia wanachama na kuzungumza nao ambao wamekiri kupata huduma nzuri hivyo tunawapongeza hawa watoa huduma kwa jitihada kubwa za uboreshaji wa huduma ambazo wanazifanya,” alisems Bw. Rutazamba.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dkt. Fred Mbwanji aliushukuru Mfuko kwa kuboresha huduma zake lakini pia kwa fursa ya mikopo nafuu ambayo imewawezesha kuboresha kwa kiwango cha juu huduma za matibabu hospitalini hapo.

“Tunajenga Wodi ya Daraja la Kwanza kwa fedha ambazo ni mkopo nafuu kabisa kutoka NHIF, lakini pia tuna mradi wa kuzalisha Maji Tiba ambao ni mkopo pia kutoka kwenye Mfuko hivyo unaweza ukaona ni kwa namna gani NHIF imekuwa ni nguzo kubwa katika uimarishaji na uboreshaji wa huduma,” alisema Dkt. Mbwanji.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi Tryphon Rutazamba akimsalimia Mama na mtoto ambao ni wanachama wa Mfuko waliokuwa wamelazwa katika Hosptali ya Wazazi Meta, Mbeya.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Uyole Mbeya Dkt. Sijabaja akitoa maelezo kwa huduma anazotoa katika hospitali hiyo. 



Hivyo makala Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya

yaani makala yote Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/uongozi-nhif-watembelea-wadau-mbeya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Uongozi NHIF watembelea Wadau Mbeya"

Post a Comment