title : UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA
kiungo : UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA
UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Tarehe mbili Desemba (Desemba 2, 2018) kuwa siku ya Uchaguzi Mdogo kwenye Jimbo la Simanjiro, Serengeti na kata 21 za Tanzania Bara.
Akitoa taarifa kwa umma Jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu Oktoba 15, 2018), Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji wa Mahakama ya Rufaa Semistocles Kaijage amesema fomu za Uteuzi wa Wagombea zitatolewa kati ya tarehe 28 Oktoba hadi 03 Novemba mwaka huu.
“Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 03 Novemba mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 04 Novemba hadi tarehe 01 Desemba mwaka huu na siku ya Uchaguzi itakuwa ni tarehe 2 Desemba, mwaka huu,” Jaji Kaijage amesema.
Mwenyekiti huyo wa Tume amesema kwamba Tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge katika Majimbo mawili (2), Jimbo la Serengeti lililopo Halmashauri ya Serengeti Mkoani Mara na Jimbo la Simanjiro katika Halmashauri ya Simanjiro Mkoani Manyara.
Jaji Kaijage alisema kwamba barua hiyo imepokelewa kufuatia Wabunge wa Majimbo hayo Waheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, na James Ole Millya kujiuzulu na kutoka kwenye Chama vyama vyao vya awali.
Amesema Tume pia imepokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa ambaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 21 za Tanzania Bara. Nafasi hizo wazi zimetokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo na kujiuzulu.
Hivyo makala UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA
yaani makala yote UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/uchaguzi-mdogo-serengeti-simanjiro-na.html
0 Response to "UCHAGUZI MDOGO SERENGETI, SIMANJIRO NA KATA 21 ZA TANZANIA BARA"
Post a Comment