title : TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR
kiungo : TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR
TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR
Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limeteua kamati mpya ndogo ya wajumbe 10 watakao simamia soka la Zanzibar kwa muda mfupi.
Akizugumza na Wandishi wa Habari katika Ukumbi wa V.I.P wa uwanja wa Amaan Raisi wa Shirikisho hilo Wallace Karia amesema kamati hiyo itakuwa na jukumu la kusimamia upatikanaji wa Katiba ya ZFA, kushughulikia shughuli zote za ZFA za Kikatiba pamoja na kutayarisha Uchaguzi mpya kwaajili ya kupatikana viongozi wapya wa ZFA.
Karia amesema kamati hiyo wameiyunda baada ya vikao vya muda mrefu baina ya pande zote na kupata muafaka wa TFF kuunda kamati hiyo ambayo itafanya kazi zake hadi Novemba 30 mwaka huu.
Kuhusu suala la kamati ya iliounda mrajisi wa vyama vya michezo Karia amesema kamati hiyo kwa sasa haitofanya kazi tena baada ya TFF kuteuwa kamati hiyo ndogo na mazungumzo baina ya TFF na mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar yalifanyika na kufahamiana vizuri.
Kamati hiyo imeundwa na wajumbe kumi wafuatao :- Mwalim Ali Mwali (Mwenyekiti), Mohamed Ali Hilali “Tedy” (Katibu), Ahmada Haji Shaabani (Mjumbe) , Rashidi Tamimu Khalfan( mjumbe), Ikram Omar Sleman( mjumbe), Salum Ubwa Nassor (Mjumbe), Rajabu Juma Mtumweni (Ujumbe), Mzee Ali Abdalla (mjumbe), Khamisi Abdalla Saidi (Mjumbe) na Mzee Ali Mzee (Mjumbe).
Baada ya kuundwa Kamati hiyo imezifuta kamati nyengine ndogo ndogo ikiwemo Kamati ya Soka la wanawake, Kamati ya Soka la Vijana (Central Taifa), Kamati ya Uchaguzi pamoja na Kamati ya Rufaa na Usuluhishi.
Hivyo makala TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR
yaani makala yote TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tff-wateuwa-kamati-mpya-itakayosimamia.html
0 Response to "TFF WATEUWA KAMATI MPYA ITAKAYOSIMAMIA SOKA LA ZANZIBAR"
Post a Comment