title : Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana
kiungo : Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana
Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana
Serikali imejipanga kuboresha upatikanaji wa ajira kwa vijana nchini kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa (Green house).
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoa wa Songea na Iringa ili kuhamasisha na kukagua maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kujenga vitalu nyumba (Green house) kwenye Mikoa hiyo.
Waziri Mhagama alisema kuwa Serikali imeamua kuanzisha mradi huo ili kuhakikisha vijana wanafikiwa kwa idadi kubwa na kuwawezesha kupata ujuzi na ajira kupitia teknolojia ya kilimo cha kisasa itakayowawezesha kujipatia kipato.
“Teknolojia hii itawawezesha vijana kulima katika eneo dogo, kupata mazao kwa wingi na kuweza kuyauza, vilevile kutumia eneo hilo kuweza kuajiri vijana wengine kwani asilimia zaidi ya 60% ya watu wanaojiajiri na kujishughulisha inatokana na na mashamba.” alisema Mhagama
Ameongeza kuwa vijana watafundishwa teknolojia hiyo ya kilimo cha kitalu nyumba ili iwawezeshe kuongeza thamani ya mazao watakayozalisha.
Aidha, Waziri Mhagama aliziagiza halmashauri zote kujipanga haraka katika utayarishaji wa miundombinu kwenye maeneo hayo na kuhakikisha vijana wanaandaliwa mapema pamoja na kuanzishiwa Vyama vya Ushirika (AMCOS) kwani wananchi wapo tayari kuona mradi huo unaanza kufanya kazi mapema.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na viongozi na watendaji (hawapo pichani) alipowasili Halmashauri ya Mufindi, Mkoani Iringa kwa ajili ya ziara ya kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo kwa Vijana na Wananchi wa Songea, alipofanya Ziara ya kikazi mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William akielezea jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoa wa Iringa kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.
Baadhi ya Viongozi na Watendaji kutoka Halmashauri ya Mufindi wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipokuwa Wilayani hapo kwa ziara ya kikazi kuhamasisha vijana na kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba. (Kulia ni) Afisa Kazi, Bi. Neema Moshi na Katibu wa Waziri Bw. Raymond Kaseko, wote kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana
yaani makala yote Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/teknolojia-ya-kitalu-nyumba-kuwakomboa.html
0 Response to "Teknolojia ya Kitalu Nyumba Kuwakomboa Vijana"
Post a Comment