title : TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA
kiungo : TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA
TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA
CHAMA cha wafanyabiashara, viwanda na kilimo nchini TCCIA ,imeweka mipango mikakati katika kutekeleza maazimio yaliyotolewa na serikali kufuatia tathimini kwamishi ya miaka mitano ambapo imelenga kuboresha shughuli mbalimbali za biashara,viwanda na kilimo.
Kimeweka utaratibu wa kuwawezesha wakulima wa korosho kwa kuwapatia nyenzo bora kwa kuwa zao hilo limechukua nafasi kubwa miongoni mwa mazao ya biashara katika kuliongezea pato Taifa kwa takribani miaka mitatu mfululizo.Maazimio hayo yalitolewa jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa bodi ya wakurugenzi wa TCCIA uliowashirikisha wadau kutoka ngazi ya kata wilaya mkoa na taifa katika kujadili masuala mbalimbali yanayowakwamisha wafanyabiashara .
Makamu wa rais TCCIA upande wa kilimoa bw. Joseph Kaungwa alisema kuwa kumejitokeza vikwazo vingi ambavyo vimechangia kukwamisha shughuli za kibashara viwanda na kilimo visisonge mbele vikiwemo kodi na tozo mbali mbali.Pia alisema kutowapa nyenzo bora pamoja na pembejeo uwezeshi na masoko ya uakika yenye kukidhi matakwa ya bidhaa zizalishwazo na wakulima ambazo kimsngi uwapatia wakati mgumu kipindi cha kuandaa mashamba na kipindi cha mavuno.
Kwa upande wake makamu wa rais TCCIA katika masuala ya biashara bwa. Julias kaijage alisema kuwa chama hicho kimeweko mifumo ya uendesheji ambayo ni bodi katika kujadili maazimio mbalimbali na kuwezesha wafanyabiashara kujipatia manufaa .
“Wakati nchi ikielekea kwenye uchumu wa kati tunawataka wafanyabiashara kuachana na masuala ya uchuuzi ambayo hayana nafasi katika kuwaletea maendelo, ‘alisema Kaijage.Nae mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mtwara Bw.Swallah Saidi alisema wamewafundisha wakulima namna ya kuifadhi korosho ili ziweze kupata bei nzuri katika soko la kimataifa ambapo itawapatia wakulima kipato cha kutosha.
“Tumezalisha zaidi ya tani laki tatu kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kuitangaza korosdho katika masoko ya nnje ambapo kurosho ya Tanzania imekuwa bora zaidi katika nchi zinazolima zao hili afrika.
Kulia ni Kaimu Rais wa Chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na Killimo (TCCIA) Octavian Mshiu akichangia baadhi ya maazimio yaliyotolewa na wanacha katika mkutano wa bodi ya wakurugenzi TCCIA jijini Dar es Salaam jana . Picha na Nicolas Gilliard.
Washiriki wakiwa katika mkutano wa bodi ya wakurugenzi TCCIA jijini Dar es Salaam jana . Picha na Nicolas Gilliard.
Baadhi washiriki wakiwa katika pica ya pamoja mara baada ya kuamaliza mkutano wa bodi ya wakurugenzi TCCIA jijini Dar es Salaam jana . Picha na Nicolas Gilliard.
Hivyo makala TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA
yaani makala yote TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tccia-yaweka-mipango-mkakati-wa-kutatua.html
0 Response to "TCCIA YAWEKA MIPANGO MKAKATI WA KUTATUA MATATIZO YA WAFANYABIASHARA"
Post a Comment