title : TCCIA YAWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA, VIWANDA,KILIMO
kiungo : TCCIA YAWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA, VIWANDA,KILIMO
TCCIA YAWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA, VIWANDA,KILIMO
Na Mwandishi wetu, Globu ya jamii
CHAMA cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini(TCCIA),imeweka mipango mikakati katika kutekeleza maazimio yaliyotolewa na Serikali ambapo imelenga kuboresha shughuli mbalimbali za biashara,viwanda na kilimo.
Kimesema kimeweka utaratibu wa kuwawezesha wakulima wa korosho kwa kuwapatia nyenzo bora kwa kuwa zao hilo limechukua nafasi kubwa miongoni mwa mazao ya biashara katika kuliongezea pato Taifa kwa takribani miaka mitatu mfululizo.
Maazimio hayo yametolewa jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCCIA uliowashirikisha wadau kutoka ngazi ya Kata,Wilaya,Mmkoa na Taifa katika kujadili masuala mbalimbali yanayowakwamisha wafanyabiashara .
Makamu wa Rais TCCIA upande wa kilimo Joseph Kaungwa amesema kuwa kumejitokeza vikwazo vingi ambavyo vimechangia kukwamisha shughuli za kibashara viwanda na kilimo visisonge mbele vikiwemo kodi na tozo mbali mbali.
Pia amesema kutowapa nyenzo bora pamoja na pembejeo wezeshi na masoko ya uhakika yenye kukidhi matakwa ya bidhaa zizalishwazo na wakulima ambazo kimsingi huwapatia wakati mgumu kipindi cha kuandaa mashamba na kipindi cha mavuno.
Kwa upande wake Makamu wa Rais TCCIA katika masuala ya biashara Julias Kaijage amesema kuwa chama hicho kimeweko mifumo ya uendesheji ambayo ni bodi katika kujadili maazimio mbalimbali na kuwezesha wafanyabiashara kujipatia manufaa .
“Wakati nchi ikielekea kwenye uchumi wa kati tunawataka wafanyabiashara kuachana na masuala ya uchuuzi ambayo hayana nafasi katika kuwaletea maendelo," amesema Kaijage.
Wakati huo huo Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mtwara Swallah Saidi amesema wamewafundisha wakulima namna ya kuhifadhi korosho ili kupata bei nzuri katika soko la kimataifa ambapo itawapatia wakulima kipato cha kutosha.
“Tumezalisha zaidi ya tani laki tatu kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kuitangaza korosho katika masoko ya nje ambapo korosho ya Tanzania imekuwa bora zaidi katika nchi zinazolima zao hili Afrika,"amesema.
Hivyo makala TCCIA YAWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA, VIWANDA,KILIMO
yaani makala yote TCCIA YAWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA, VIWANDA,KILIMO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCCIA YAWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA, VIWANDA,KILIMO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tccia-yaweka-mikakati-kuboresha-sekta.html
0 Response to "TCCIA YAWEKA MIKAKATI KUBORESHA SEKTA YA BIASHARA, VIWANDA,KILIMO"
Post a Comment