title : TANZANIA YASHRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI ,GENEVA USWISI.
kiungo : TANZANIA YASHRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI ,GENEVA USWISI.
TANZANIA YASHRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI ,GENEVA USWISI.
*Tanzania ni kati ya nchi 160 zinazoshiriki Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji.
Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji (World Investment Forum) limefunguliwa tarehe 22 Oktoba 2018 Geneva, Uswisi na Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) Dkt. Mukisa Khitui na litaendelea mpaka Oktoba 26,2018.
Kauli mbiu ya kongamnao ni ‘uwekezaji kwa maendeleo endelevu’ (investing for sustainable development) ambapo majadiliano yatajikita kwenye changamoto za uwekezaji katika mazingira mapya ya utandawazi na mapinduzi ya viwanda (Globalization and Industrialization).
Kongamano hili la aina yake huandaliwa kila baada ya miaka miwili na UNCTAD kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Uwekezaji. Takribani washiriki zaidi ya 5,000 wanashiriki kutoka nchi 160 duniani ikiwemo Tanzania na ujumbe wake unaongozwa na Balozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Geneva, Dkt. James Alex Msekela.
Washiriki wa kongamnao hilo ni kutoka katika nyanja mbalimbali za umma na sekta binafsi ikiwamo Wakuu wa nchi, Mawaziri Wakuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi za Uwekezaji. Wengine ni Watendaji wa Makampuni ya Kimataifa na Ushirikiano wa Hisa, Wasimamizi wa Mifuko ya Fedha, Wakurugenzi Wakuu wa Mashirika ya Sekta Binafsi, Wataalam wa eneo la Uwekezaji wa Kimataifa,Wabunge,Wawakilishi wa Vyama vya Kiraia, Wasomi Maarufu, na vyombo vya Habari vya Kimataifa.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kama mdau wa masuala ya uwekezaji nchini kinashiriki katika kongamano hili ambapo Mkurugenzi Mtendaji Bw. Geoffrey Mwambe atashiriki katika vipindi/midahalo na majadiliano mbalimbali kwa lengo la kuinadi Tanzania kuwa ni nchi bora ya kuwekeza Afrika kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo amani, uchumi imara unaokua kwa kasi, uwepo wa rasilimali, uwepo wa miundo mbinu na uongozi bora.
Mhe Balozi Dkt. James Msekela (wa tatu kutoka kulia) na Mkuregenzi wa TIC Bw. Geoffrey Mwambe (wa ili kutoka kulia) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa uwekezaji Geneva,Uswisi.
Rais wa Namibia Mhe.Dkt Hage Geingob akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Geoffrey Mwambe katika Banda la Tanzania kwenye kongamano la kimataifa la Uwekezaji.
Ufunguzi wa kongamano la Kimataifa la Uwekezaji.
Hivyo makala TANZANIA YASHRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI ,GENEVA USWISI.
yaani makala yote TANZANIA YASHRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI ,GENEVA USWISI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YASHRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI ,GENEVA USWISI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tanzania-yashriki-kongamano-la.html
0 Response to "TANZANIA YASHRIKI KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UWEKEZAJI ,GENEVA USWISI."
Post a Comment