title : Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia
kiungo : Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia
Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia
Na Mwandishi Wetu, aliyekuwa Lilongwe, Malawi
TAASISI zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mikopo kutoka kwa wanufaika na hivyo kuongeza uwezo wa taasisi hizo kutoa mikopo kwa wahitaji wengi zaidi.
Bw. Alex Twinomugisha, Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa kampuni ya TEHAMA ya Intel, amewaambia wiki iliyopita (Sept 27, 2018) Watendaji Wakuu wa taasisi hizo na wadau wengine wanaokutana mjini Lilongwe kuwa matumizi ya TEHAMA hayana mjadala katika kuongeza ufanisi.
Mkutano huo umeandaliwa na Shirikisho la Taasisi za kiserikali zinazotoa Mikopo ya Elimu ya Juu Afrika ambazo (AAHEFA).
Taasisi zilizoshiriki mkutano huo zinatoka katika nchi za Malawi, Botswana, Ghana, Kenya na Lesotho. Nchi nyingine zilizoshiriki ni Rwanda, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Tanzania.
“Swali mnalopaswa kujiuliza kila mara ni – mnafanya nini tofauti na mwaka jana au miaka iliyopita kuhusu matumizi ya TEHAMA?”, aliuliza na kuongeza kuwa taasisi hizo zinapaswa kuongeza matumizi ya TEHAMA katika kutoa huduma bora kabla ya wateja wao hawajalalamika.
“Zaidi ya asilimia 50 ya kazi hivi sasa zinahitaji matumizi ya TEHAMA na katika baadhi ya nchi zenu, kama Kenya, kwa mfano, takribani theluthi moja ya makusanyo ya mikopo iliyoiva yanapatikana kupitia huduma ya simu za mkononi… ni huduma rafiki na rahisi,” amesema Bw. Twinomugisha wakati akiwasilisha mada iliyoitwa ‘Mapinduzi ya Nne ya Soko la Ajira: Elimu ya sasa inawezaje kutatua?”.
Katika mkutano huo, washiriki pia walipata fursa ya kusikiliza na kujadili mada iliyohusu ‘Kuunganisha Mifumo ya Taasisi za Mikopo ya Elimu ya Juu ili Kuimarisha Makusanyo – Kuongeza Matumizi ya Kidigitali’ iliyowasilishwa na Bw. Charles Odour, mtaalamu kutoka kampuni ya ushauri ya Ernest & Young.
Katika mada yake, Bw. Odour alizungumzia umuhimu wa taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu kuanzisha mifumo itakayohakikisha kila mnufaika wa mkopo anapatikana kwa urahisi na kuanza kurejesha bila kujali mahali alipo duniani popote.
“Dunia hivi sasa inaendeshwa kidigitali, tunawasiliana na wateja kidigitali … na nyie mna taarifa nyingi kuhusu wateja wenu, mnachotakiwa kufanya ni kuanzisha mifumo itakayobaini wanufaika ili waanze kurejesha,” amesema Bw. Odour.
Akichangia mada ya Bw. Odour, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Kenya Bw. Charles Ringera amesema ili taasisi za zinazotoa mikopo ya elimu ya juu ziweze kukusanya mikopo kwa ufanisi, hazina budi kuhakikisha kanzidata zao zinaunganishwa na mifumo mingine ya wadau muhimu.
“Kwa Kenya, tumeunganisha mfumo wetu na mingine muhimu kama ile ya mamlaka ya mapato, mfumo wa bima ya afya, wa mamlaka ya usafiri na mingine … kwa hiyo ikitokea mnufaika wa mkopo anahudumiwa na taasisi moja, na sisi tunapata taarifa na kuanza kumdai iwapo hajaanza kurejesha,” amesema Bw. Ringera ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Taasisi za Serikali zinatoa mikopo ya Elimu ya Juu Afrika (AAHEFA).
Akichangia mada hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Tanzania (HESLB) Bw. Abdul-Razaq Badru amesema HESLB inatambua umuhimu wa TEHAMA katika kuboresha ufanisi na kuwa hivi sasa ipo katika maboresho makubwa na mifumo yake ya ndani ili iweze kuunganishwa na mifumo ya nje na hivyo kuongeza ufanisi.
“Hivi sasa tunaboresha mifumo yetu uombaji, upangaji na ukusanyaji wa mikopo na baada ya hapo, itaweza ‘kuongea’ na mifumo ya nje ya wadau wengine na hivyo kutoa huduma bora kwa wateja wetu,” amesema Bw. Badru.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu wa Mutharika na umefungwa mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Malawi Bw. Justin Saidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Abdul-
Razaq Badru akiongea katika mkutano uliojumuisha Watendaji Wakuu, maafisa na wadau wa taasisi
zinazotoa mikopo ya elimu barani Afrika hivi karibuni mjini Lilongwe, Malawi.
Baadhi ya Watendaji Wakuu wa taasisi zinazotoa mikopo ya elimu Afrika katika moja ya vikao vya mkutano ulioshirikisha taasisi hizo hivi karibuni mjini Lilongwe, Malawi.
Hivyo makala Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia
yaani makala yote Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/taasisi-zinazotoa-mikopo-ya-elimu-ya.html
0 Response to "Taasisi zinazotoa mikopo ya elimu ya juu barani Afrika zimehimizwa kuongeza matumizi ya teknolojia"
Post a Comment