title : SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA
kiungo : SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA
SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA
Na Khadija Seif, Blogu ya Jamii
KAMPUNI ya mchezo wa kubashiri ya sportpesa imechezesha droo ya 28 ya promosheni ya shinda zaidi na sportpesa, ambapo Amri Nicolas(28) kutoka Kigoma ameibuka mshindi wa Bajaji RE.
akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa sportpesa Abass Tarimba ameeleza kuwa kuna ongezeko kubwa la zawadi Kwenye promosheni hiyo.
Tarimba ameeleza kuwa wachezaji wa sportpesa kupitia mitandao yote wana nafasi ya kushinda zawadi mpya .
Amesema kuwa zawadi hizo zikiwemo smartphone, jezi za klabu ya Simba au Yanga pamoja na tiketi ya kuhudhuria mechi za ligi ya hispania na Uingereza kila mwezi.
Tarimba amesema kuwa kutokana na ukubwa wa promosheni hiyo kwa sasa wameamua kuongeza zawadi zitakazotoka kila wiki na kila mwezi na
Ongezeko hilo la zawadi limewekwa kwa lengo la kuhamasisha wateja waweze kushiriki na kushinda zawadi mbalimbali kupitia mchezo huo wa kubashiri.
Amefafanua pia wateja waendelee kubashiri kwa wingi ili kujiweka Kwenye nafasi ya ushindi mnono ambapo unaweza kucheza kupitia mitandao yote, na mpaka sasa washindi kutoka Mikoa 13 wamepatikana ikiwemo Dar es salaam, Kigoma, Mwanza,Tanga, Singida, Ruvuma , Morogoro, Iringa, Kahama, Songwe, Mbeya, Pwani na Lindi.
Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa sportpesa Abass Tarimba(kulia) pamoja na Mtangazaji wa Kipindi cha shinda zaidi na SportPesa Happiness Wandela(kushoto) wakionyesha Jezi ya Yanga kama zawadi kwa mshindi wa Promosheni ya Sinda na Sportpesa ambayo inatoa zawadi hizo zikiwemo smartphone, tiketi ya kuhudhuria mechi za ligi ya hispania na Uingereza kila mwezi.
Mtangazaji wa Kipindi cha shinda zaidi na SportPesa Happiness Wandela(kushoto) akizungumza na mmoja wa shindi wa shindano hilo leo. Kulia ni Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa sportpesa Abass Tarimba
Hivyo makala SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA
yaani makala yote SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/smartphone-jezi-na-tiketi-kutolewa-kwa.html
0 Response to "SMARTPHONE, JEZI NA TIKETI KUTOLEWA KWA WASHINDI WA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA"
Post a Comment