PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU

PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU
kiungo : PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU

soma pia


PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU


Serikali imeitaka Bodi ya Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kuhakikisha inaboresha miundombinu ya chuo na kuzingatia miiko na kanuni za ufundishaji ili wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo waweze kukidhi mahitaji ya soko.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati akizindua bodi hiyo na kusisitiza kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha majengo kwa kutangaza zabuni kwa uwazi ili kuepuka mianya ya rushwa.

“Hakikisheni mnakuwa na mpango madubuti wa kuboresha majengo ya chuo ili chuo kibaki na hadhi yake, lakini pia hakikisheni mntoa elimu bora kwa wanafunzi wanaokuja kusoma hapa ili waweze kupata misingi imara itakayowawezesha kuajiriwa ndani na nje ya nchi mara baada ya kuhitimu masomo yao”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa Serikali ina uhitaji wa wataalam wengi kwenye masuala ya bahari hivyo ni wajibu wa bodi kusimamia chuo na kuhakikisha wataalam hao wanazalishwa kwa wingi chuoni hapo ili kukidhi mahitaji ya soko kitaifa na kimataifa.

Amewataka wakufunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanatumia lugha nzuri kwenye ufundishaji ili kuwaweka wanafunzi karibu na kuhakikisha wanapata taaluma inayotakiwa kwani kuwepo kwa waalimu hao kunategemea kuwepo kwa wanafunzi.

“Ni lazima tufungue milango kwa wanafunzi sababu wapo wanaoelewa haraka na wanaoelewa taratibu, hivyo tukae nao muda mrefu ili kubaini changamoto zao lakini pia tuwe waangalifu juu ya matumizi ya lugha tunazotumia kwa wanafunzi wakati tunapofundisha”, amefafanua Prof. Mbarawa.


Hivyo makala PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU

yaani makala yote PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/prof-mbarawa-aitaka-bodi-ya-dmi_23.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU"

Post a Comment