SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE

SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE
kiungo : SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE

soma pia


SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE

Mwambawahabari
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) (kushoto) akiungana na viongozi wa Halmashauri ya Chamwino Mkoani Dodoma katika kupuliza kipenga cha kuashiria uzinduzi wa awali wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wanawake wa Vijijini kuandaliwa kwa mara ya kwanza hapa nchini katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Mwandishi Wetu Dodoma
Serikali imehimiza jamii ya watanzania kutokomeza mila na desturi kandamizi na zenye madhara ili kuwawezesha wanawake, wasichana pamoja na jamii yote inayoishi vijijini kunufaika na miundombinu na huduma za kijamii na kiuchumi zinazoendelea kuboreshwa hapa nchini
Hayo yamesemwa leo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John JIngu alipokuwa akihutubia wanawake na wasichana waishio vijijini kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Ally Mwalimu (Mb.) katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanamke wanaoishi vijijini iliyofanyika kwa mara ya kwanza kitaifa mkoani Dodoma katika kijiji cha Manchali B, Kata ya Manchali wilayani Chamwino.
Dkt. Jingu amesema kuwa kwa mwaka huu Kaulimbiu ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Wanaoishi Vijijini inasema  Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Miundombinu, Huduma za Jamii kwa Wanawake na Wasichana Wanaoishi Vijijini”   na imezingatia vipaumbele vya kitaifa na muktadha wa nchi yetu na msisitizo mkubwa amabao umewekwa katika kufikia uchumi wa viwanda na maendeleo ya watu hususan wanawake na wasichana wanaoishi vijijini kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na  Mpango wa Taifa wa Pili wa Maendeleo 2015/16 – 2020/21 pamoja na Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto 2016/17 – 2021/22.

Ameongeza kuwa maadhimisho hayo yamewaleta pamoja wanawake, wanaume, wasichana na wanaume wanaoishi kijijini wakiwemo watunga Sera, Asasi za Kiraia, wadau wa maendeleo na Taasisi Binafsi kwa lengo la kutafakari na kujadili kuhusu fursa na changamoto za Mwanamke anayeishi kijijini.

Dkt. Jingu ameisisitiza jamii kutambua na kuthamini mchango wa kundi hilo hususan katika kuimarisha uchumi wa viwanda na maendeleo ya kilimo pamoja na kuchukua hatua za makusudi za kuboresha hali ya wanawake na wasichana wanaoishi vijijini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Vumilia Nyamoga amesema kuwa kupitia maadhimisho haya wanawake wanaoishi kijijini watapata nafasi ya kufahamu jitihada zinazofanywa na Serikali na wadau mbalimbali na pia watapata fursa ya kutoa mrejesho wa namna ya kuboresha afua na huduma hizo.
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UN Women) Bi. Hodan Addou ameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwasaidia wanawake na wasichana waishio vijijini kutafakari, kutathmini na kutumia ipasavyo fursa zinazotokana na jitihada za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali na wadau mbalimbali ikiwemo uwezeshaji wa wanawake kiuchumi, uboreshaji wa huduma za afya, uboreshaji wa miundombinu ya usafiri ikiwemo barabara, uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za umeme vijijini.

Aidha  Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Bw. Julius Mbilinyi amesema kuwa wanawake wa kijijini ni nguzo ya familia na taifa kwa ujumla kwani kwa asilimia kubwa maendeleo ya nchi yanaletwa na wanawake hasa wanawake waishio vijijini.


Naye mmoja wa wanawake wa kijiji cha Manchali kilichopo wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Bi. Rose Masima ameiomba Serikali kuwasaidia wananwake wa kijijini kupata mikopo kutoka mfuko wa wanawake WDF kwani imekua bado haiwafikii wanawake hao.


Hivyo makala SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE

yaani makala yote SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/serikali-yahimiza-jamii-kutokomeza-mila.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAHIMIZA JAMII KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WANAWAKE"

Post a Comment