SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA

SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA
kiungo : SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA

soma pia


SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA


Na Anitha Jonas – WHUSM – Hydom,Manyara. 

Serikali imejipanga kuanzisha programu ya kukusanya na kuhifadhi taarifa jamii za kitanzania ambazo asili ya utamaduni wake upo hatarini kupotea. 

Kauli hiyo imetolewa leo katika Kijiji cha Hydom,Wilaya ya Mbulu Vijijini, Mkoani Manyara na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi alipokuwa akifunga Tamasha la Saba la Utamaduni wa Pembe Nne (7th Four Corner Cultural Festival) kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ambaye ndiye alikuwa afunge tamasha hilo. 

Bi.Mlawi alitoa pongezi kwa waandaaji wa tamasha hilo linahusisha makundi manne ya lugha yanayopatikana barani Afrika ila kwa Tanzania yanapatikana mkoani Manyara na jirani ambapo kwa sasa yameanza kupoteza asili yao na utamaduni wake ambayo ni Wahdzabe-Khoisan,Iraqw-Cushits,Datooga-Nilotic na Wabantu-Wanyiramba/ Wanyisanzu. 

“Kupitia Idara ya Utamaduni iliyo chini ya Wizara hii nitaunda Kitengo kitakacho kuwa kinashughulikia suala la ukufanyaji wa taarifa za makabila mbalimbali nchini katika mfumo wa picha jongefu pamoja na uandishi wa historia fupi makabila hayo kwa lengo la kuweza kuhifadhi taarifa hizo kwa maslai ya vizazi vijavyo”alisema Bi.Mlawi. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi akipongeza uongozi wa Four Corner Cultural Programme (4CCP) kwa kuendesha lenye kuenzi Utamaduni,Mila na Desturi za makabila manne yanayopatikana barani Afrika ambayo niyakujivunia leo katika sherehe za kufunga tamasha hilo lililofanyika katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi akimkabidhi cheti cha ushiriki muwakilishi wa Taasisi ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw.Gibson Ngolongolo leo katika sherehe za kufunga tamasha la saba la 4CCP lililofanyika katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini .
Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe.Flatei Massey na Mratibu wa Kituo cha Four Cultural Programme Bi.Eliminata Awet wakiwa wamejiwekea nyoka mabegani anayetumika kuchezea ngoma ya kikiundi cha wasukuma kutoka Mwanza wakati wa Sherehe za Kufunga Tamasha la Four Corner Cultural Festival liloandaliwa na 4CCP na kufanyika leo katika Kijiji cha Hydom Wilaya ya Mbulu Vijijini,wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi.
Baadhi ya Vijana kutoka Jamii ya Kidatooga wakicheza ngoma ya asili ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Suzan Mlawi(hayupo pichani) katika himaya ya nyumba yao iliyopo katika kituo cha makumbusho ya Four Corner Cultural Programme (4CCP) leo katika sherehe za kufunga tamasha la saba la Four Corner Cultural Festival lililofanyika Kijiji cha Hydom,Wilaya ya Mbulu Vijijini.


Hivyo makala SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA

yaani makala yote SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/serikali-kuhifadhi-utamaduni-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI KUHIFADHI UTAMADUNI WA MAKABILA YALIYO HATARINI KUPOTEA"

Post a Comment