RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO

RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO
kiungo : RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO

soma pia


RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO

NA TIGANYA VINCENT, RS TABORA.

VIONGOZI wa kuanzia ngazi za Kata hadi vijiji na Shule zote wametakiwa kuandaa orodha ya watoto ambao bado ni watoro na kuziwasilisha ngazi za juu ili wao na wazazi wao waweze kuchukuliwa hatua kwa kudai amri halali ya Serikali ya kuwataka kuwa madarasani toka mwezi Julai mwaka huu. Agizo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa.

Alisema kwa takwimu za hivi karibuni ni watoto 6,206 kati ya 11,004 ambao walikuwa watoro ndio wamerudi darasani kwa ajili ya kuendelea na masomo kama alivyokuwa ameagiza. Mwanri alisema watoto waliorudi ni zaidi ya asilimia 50 na waliobaki wanaofikia 4,998 na kutaka waanze mara moja kutafutwa walipo kwa ajili ya kurudishwa madarasani.

Alisema hakuna sababu ya kufanya mzazi ashindwe kumpeleka shule mtoto wake kwani Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeondoa vikwazo vyote vilivyokuwa vikisababisha ugumu kwa mzazi.

Mwanri alisema Mwalimu , Afisa Elimu Kata na Mtendaji wa Kata akishindwa kuchukua hatua atalizika kuchukuliwa hatua yeye kama kikwazo cha kukwamisha jitihada za Mkoa za kuondoa utoro, ziro na utumishaji watoto katika mashamba ya tumbaku na migodini.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka walimu Mkoani humo kufanyakazi kama chaja ili wasaidie katika unoaji na uibuaji wa vipaji vya wanafunzi kuanzia msingi hadi Sekondari kwa ajili ya maendeleo ya Tabora.

Alisema hatua hiyo itasaidia kurudisha historia ya Mkoa wa Tabora wa kuwa chimbuko la wasomi na viongozi watakaoshika nyadhifa mbalimbali hapa nchini.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema kuwa wao ndio wasimamizi wakuu wa elimu katika maeneo yao ni vema wakazingatia kampeni ya Mkoa wa Tabora inayosema Tabora bila sifuri,utoro, utumikishaji watoto mashambani, na mimba za utotoni inawezekana kila mmoja atimize wajibu wake.

Aidha aliwataka kuhakikisha wanaboresha mazingira ya shule kwa kupanda miti na maua ili kuwavutia watoto wapende kujifunza.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa leo mjia hapa. Wengini ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu(wa pili kutoka kushoto) , Kaimu Katibu Tawala Msaidizi(Utawala na Utumishi) Aidan Lucas(kulia) na Afisa wa Serikali za Mitaa Shukuru Kazembe(kushoto).
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maelezo mafupi wakati kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa leo mjini hapa.
Afisa Elimu Mkoa wa Tabora Susan Nussu akitoa maelezo mafupi wakati kikao kazi cha siku moja cha Maofisa Elimu Kata, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Wakuu wa Shule za Sekondari kutoka Wilaya ya Sikonge, Uyui na Tabora Manispaa leo mjini hapa.


Hivyo makala RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO

yaani makala yote RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/rc-tabora-aagiza-kupewa-orodha-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RC TABORA AAGIZA KUPEWA ORODHA YA WATOTO AMBAO BADO NI WATORO"

Post a Comment