title : NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI
kiungo : NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI
NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI
*Ni baada ya kubaini kufanya udanganyifu, yatangaza kurudiwa kwa mtihani
Na Ripota Wetu, Globu ya Jamii
HATIMAYE Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuyafuta matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa shule za msingi zote zilizopo ndani ya Halmashauri ya Chemba mkoani Dodoma, pamoja na baadhi ya shule zilizopo katika halmashauri ya Ubungo, Kinondoni, Kondoa na Mwanza.
Kwa mujibu wa Necta imeamua kufuta matokeo ya shule hizo baada ya kubaini kuvuja kwa mtihani huo katika shule hizo na kwamba hilo ni jambo ambalo ni kinyume na sheria na kanuni za mitihani nchini kwetu.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) Charles Msonde ametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam ambapo amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuvunjwa kwa kanuni za mitihani baraza hilo limeamua kufuta matokeo ya mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi katika shule za msingi za halmashauri hizo.
"Hivyo watahiniwa wote watarudia tena mtihani huo Oktoba 8 na 9 mwaka huu kwa halmashauri zote ambazo halmashauri zao uchaguzi umefutwa baada ya kubaini umevuja," amesema Dk.Msonde.
Ametaja shule ambazo zimefutiwa matokeo ya mtihani imo Shule ya Msingi Hazina na New Hazina zilizopo Magomeni wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pia Shule ya Aniny Nndumi na Fountain of Joy zilizopo Ubungo, Shule ya Msingi Kondoa Integrity iliyopo Halmashauri ya Kondoa, pamoja na Shule ya Msingi Kisiwani, Alliance na New Alliance zilizopo Mwanza.
Dk.Msonde amesema pia baraza hilo limefuta vituo vya mitihani kwa shule nane ambazo zilihusika katika uvujishaji wa mitihani hiyo sambamba na kupendekeza kuondolewa kwenye nafasi za ajira kwa baadhi ya maofisa elimu kata na wilaya waliohusika kwenye udanganyifu huo.
Amefafanua Necta wameidhinisha vituo mbadala vya mtihani vitakavyotumiwa na watahiniwa katika mtihani wa marudio utakaoufanya Ocktoba 8 na 9 wiki ijayo.
" Shule ya Msingi Hazina na New Hazina wanafunzi wake wa darasa la saba watafanya mtihani huo katika shule ya Msingi Osterbay.
" Shule ya Fountain of Joy na Aniny Nndumi za Ubungo zitafanya mtihani katika shule ya Msingi Mbezi.Shule ya Msingi Kisiwani ya jijini Mwanza wanafunzi wake watafanya mtihani huo kwenye shule ya Msingi Kakebe.
"Shule ya Alliance na New Alliance watahiniwa watafanya mtihani katika shule ya Msingi Mahina na Shule ya Msingi ya Kondoa Integrity wanafunzi watafanya mtihani kwenye shule ya Msingi Bicha, " amefafanua.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI
yaani makala yote NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/necta-yafuta-matokeo-ya-mtihani-wa.html
0 Response to "NECTA YAFUTA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA KWA BAADHI YA SHULE ZA MSINGI NCHINI"
Post a Comment