title : Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP
kiungo : Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP
Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.JALADA la kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani milioni 3.7, sawa na Sh.bilioni nane, dhidi ya vigogo wanne wa Kampuni ya Six Telecoms Limited na kampuni yenyewe limetua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai (DPP).
Mwendesha mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.
Hatua hiyo imefika baada ya Kishenyi kuieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Kutokana na taarifa hiyo, wakili wa utetezi Alex Mgongolwa aliomba kujua upelelezi dhidi ya kesi hiyo umefikia wapi.
"Mheshimiwa, jalada la kesi hii liko kwa DPP, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa", amedai Kishenyi.
Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mhandisi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Six telecoms, Hafidhi Shamte, Mfanyabiashara na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Peter Noni, Mwanasheria na Mhadhiri na Mkurugenzi wa hiyo kampuni Dkt ,Ringo Tenga, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo Noel Chacha na Kampuni ya Six Telecoms Limited.
Wote kwa pamoja wanadaiwa kuhujumu miundombinu ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa kutoza garama chini ya kiwango, kushindwa kulipa ada za udhibiti na kutakatisha 3,282,741.12.
Pia washtakiwa hao wanadaiwa kuisababishia TCRA hasara ya USD 3,748,751.22, sawa na Sh 8 bilioni za kitanzania.
Hivyo makala Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP
yaani makala yote Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/01/jalada-la-kesi-ya-vigogo-six-telecom.html
0 Response to "Jalada la kesi ya Vigogo, Six telecom latua kwa DPP"
Post a Comment