MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI

MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI
kiungo : MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI

soma pia


MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR

MWAKILISHI mteule wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Jang’ombe Ndugu Ramadhan Hamza Chande leo amekabidhiwa rasmi Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa nafasi ya Uwakilishi wa Jimbo hilo.

Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Mjini iliyopo Maisara na kuudhuriwa na Viongozi na Wanatendaji wandamizi Tume hiyo na CCM.Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Mwakilishi mteule huyo Ramadhan Hamza ameahidi kufanya kazi kwa uadilifu na kwa kufuata miongozo na taratibu zote za kisheria kwa maslahi ya wananchi wote wa Jimbo hilo. 

Amewashukuru wananchi na wanachama wa CCM wa Jimbo hilo kwa kumpatia ridhaa yangu kuongoza Jimbo hilo kupitia utaratibu halali wa kidemokrasia. “Nitawatumikia kwa uadilifu wananchi wote wa Jang’ombe bila ya ubaguzi wowote kwani naamini bila yenu nyinyi kuridhia kunipa nafasi hii nisingeweza kushinda katika mchakato huu wa kisiasa uliokuwa na ushindani mkubwa.Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 tayari nishakabidhiwa muda wowote nitaanza kutekeleza mpango kazi wangu kwa lengo la kutekeleza ahadi nilizoahidi katika kampeni.”,ameeleza Chande.

Kwa upande wake aliyekuwa Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Jang’ombe ambaye pia ni Afisa wa ZEC Wilaya ya Mjini Bi.Mwanapili Khamis Mohamed amemsisitiza kiongozi huyo kufanya kazi zake kwa majibu wa taratibu na kanuni za kisheria ili kutimiza matakwa ya wananchi waliomchagua. 

Mwakilishi huyo aliyeshinda nafasi hiyo jana kwa kura 6,581 sawa na asilimia 90.5 katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe uliofanyika kwa amani bila ya kujitokeza matukio ya uvunjifu wa sheria za Uchaguzi na nchi kwa ujumla.
AFISA wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Mjini Mwanapili Khamis Mohamed (kulia) akimkabidhi Cheti cha udhibitisho wa Ushindi wa nafasi ya Uwakilishi Mwakilishi mteule wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande (kushoto) , aliyekuwa Wakala wa Mgombea wa CCM katika Uchaguzi huo Rajab Uweje Yakoub (wa pili kushoto).
ALIYEKUWA Wakala wa Mgombea Uwakilishi wa CCM Ndugu Rajab Uweje Yakoub (wa pili kushoto) akisaini Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa Uwakilishi cha Mwakilishi mteule wa CCM Jimbo la Jang’ombe.
MWAKILISHI mteule wa Jimbo la Jang’ombe Ramadhan Hamza Chande akionyesha Cheti cha udhibitisho wa ushindi wa Uwakilishi kupitia Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo uliofanyika Jana.



Hivyo makala MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI

yaani makala yote MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/mwakilishi-mteule-wa-jangombe.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWAKILISHI MTEULE WA JANG’OMBE AKABIDHIWA CHETI CHA USHINDI"

Post a Comment