title : Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma
kiungo : Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma
Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma
Na John Stephen, Musoma
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeongeza siku saba zaidi kwa watalaam wake walioko Hospitali ya Rufaa Musoma ili kuhakikisha wanahudumia idadi ya wananchi wengi waliojitokeza kwa wingi kupata huduma katika kambi maalumu iliyoanza Oktoba 7, 2018 mkoani Mara.
Kambi hiyo ilitarajiwa kuisha leo Oktoba 12, 2018, lakini kutokana na hitaji kubwa la wananchi waliojitokeza kupata huduma, uongozi wa hospitali umeamua kuongeza siku hadi Ijumaa ijayo tarehe 19 Oktoba, 2018 ambapo watahitimisha na kurejea jijini Dar es Salaam.
Hadi kufikia jana Alhamisi jumla ya wananchi 1210 walikuwa wamejiandikisha kupata huduma mbalimbali za matibabu kati hao wananchi 1155 wameonwa na watalaamu wa Muhimbili wale wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Musoma.
Kati ya hao, kinamama watano wamefanyiwa upasuaji, 36 wenye matatizo ya macho wamepatiwa huduma ya upasuaji, wagojwa wanane wamepatiwa huduma ya upasuaji wa mfumo wa mkojo, 14 upasuaji wa magonjwa mbalimbali (general surgery), 10 upasuaji wa masikio, koo na pua na 233 wamefaniwa uchunguzi wa kawaida.
Baadhi ya wagonjwa wamepewa rufaa za kwenda kutibiwa Muhimbili na wengine Hospitali ya Bugando ambako watafanyiwa uchunguzi zaidi na hatimaye kupata tiba stahiki kutokana na mazingira ya ugonjwa.
Hospitali ya Taifa Muhimbili ilipeleka watalaam wake 14 mkoani Mara katika Hospitali ya Rufaa ya Musoma mapema wiki hii ili kujenga uwezo wa watalaam na kutoa huduma kwa wananchi wenye matatizo mbalimbali ya afya.
Wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakishirikiana na wataalam wa Hospitali ya Rufaa Musoma kufanya upasuaji kwa mgonjwa mwenye tatizo katika mfumo wa mkojo. Kutoka kulia ni mtaalamu wa chumba cha upasuaji, Anna Msafiri, Dkt. Isaack Mlatie, Dkt. Paul Masua na Dkt. Masanja.
Dkt. Athuman Mbalamula wa Muhimbili akifanya upasuaji kwa mgonjwa mwenye tatizo sehemu ya tumbo kwa kushirikiana na mtaalamu wa upasuaji, Joram Laurent wa Hospitali ya Rufaa Musoma.
Mmoja wa mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Musoma akionwa na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani wa Muhimbili, Dkt. Brighton Mushengezi kwa kushirikiana na Mtaalam wa magonjwa ya ndani, Farbian Gabriel Beyesigwa wa Hospitali ya Rufaa Musoma.
Daktari bingwa wa macho wa Muhimbili, Dkt. Neema Kanyaro akitoa huduma ya macho kwa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa macho leo katika Hospitali ya Rufaa Musoma.
Mmoja wa watoto wenye tatizo kwenye koo akifanyiwa upasuaji leo na daktari bingwa Muhimbili, Dkt. Raymond Leiya.
Wataalam wa upasuaji wa Hospitali ya Rufaa Musoma wakifanya upasuaji kwa kushirikiana na wataalam wa Muhimbili Dkt. Athuman Mbalamula na Dkt. Helen Mrina.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma
yaani makala yote Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/muhimbili-waongeza-siku-saba-kuhudumia.html
0 Response to "Muhimbili waongeza siku saba kuhudumia Wananchi Musoma"
Post a Comment