MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI

MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI
kiungo : MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI

soma pia


MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan.

Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania ,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi  Mkoani Pwani  leo oktoba 24 ambapo atatembelea miradi mikubwa ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo.

Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa  wa Pwani,  Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari .

Ndikilo amesema ,makamu wa Rais akiwa mkoani humo  atakagua miradi  mbalimbali   ya maendeleo katika Wilaya  nne za mkoa huo na ataanzia ziara kwa kukagua miradi ya maendeleo ya Wilayani Bagamoyo.

"Miradi hiyo ni pamoja na kutembelea   mradi mkubwa wa  Bandari mpya ya Mbegani wilayani Bagamoyo  yenye ubia  na nchi tatu za Tanzania,Oman na China," alisema Ndikilo.

Amesema kuwa baada  ya kukagua miradi wilayani Bagamoyo atakwenda  Halmashauri ya wilaya ya Chalinze  ambako atakagua miradi ya maendeleo.

 "Baada ya hapo atakwenda , Wilaya ya Kisarawe, Mkuranga na atahitimisha ziara hiyo wilaya ya Kibaha"

Aidha mradi mwingine wa kitaifa ni atakaotembelea ni ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR) kwenye karakana kubwa iliyoko Soga wilayani Kibaha.

"Mbali ya kutembelea miradi hiyo mikubwa pia atatembelea miradi mingine ikiwemo ya miradi ya  afya,  maji na elimu,"alisema Ndikilo.

Ndikilo alisema kuwa akiwa wilayani Kibaha Makamu wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya wiki ya viwanda itakayozinduliwa Oktoba 29 katika viwanja vya Sabasaba vilivyopo  katika eneo la Picha ya Ndege.

Makamu wa Rais atakapoanza ziara hiyo  atapokea taarifa kutoka  Halmashauri zote  za mkoa huo pia atapata nafasi ya kuzungumza na  Wakurugenzi wa Halmashauri hizo.


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/makamu-wa-rais-kuanza-ziara-ya-kikazi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS KUANZA ZIARA YA KIKAZI MKOANI PWANI"

Post a Comment