title : Freeman Mbowe, Ester Matiko Walivyodishwa Gereani ,Baada Ya Serikali Kukata Rufaa
kiungo : Freeman Mbowe, Ester Matiko Walivyodishwa Gereani ,Baada Ya Serikali Kukata Rufaa
Freeman Mbowe, Ester Matiko Walivyodishwa Gereani ,Baada Ya Serikali Kukata Rufaa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imesimamisha kwa muda mwenendo wa kesi iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko hadi rufaa iliyofunguliwa na jamhuri katika Mahakama ya Rufaa utakapotolewa.
Mbowe na Matiko, walifungua maombi ya pingamizi kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuwafutia dhamana kwa kukiuka masharti.
Jana, upande wa Jamhuri uliwasilisha maombi mahakamani hapo kutaka maombi hayo yatupwe kutoka na kukiuka baadhi ya sheria katika maombi yao hata hivyo Jaji Sam Rumanyika alitupilia mbali ombi hilo na kusikiliza shauri hilo.
Akisoma uamuzi huo mahakamani hapo leo Ijumaa Novemba 30, Jaji Rumanyika, amesema upande wa jamhuri ulifungua maombi ya kupinga uamuzi wa Jaji Rumanyika wa kupinga usikilizaji wa hatua ya rufaa.
Alisema sheria inampa mamlaka Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kufungua maombi ya kupata rufaa wakati shauri likiendelea kwa ngazi ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.
“Mahakama Kuu imesimamisha mwenendo wa kesi iliyofunguliwa na upande wa utetezi wakipinga uamuzi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kuwafutia dhamana, kesi hiyo itaendelea baada ya Mahakama ya Rufaa kutoa uamuzi,” amesema Jaji Rumanyika.
Hivyo makala Freeman Mbowe, Ester Matiko Walivyodishwa Gereani ,Baada Ya Serikali Kukata Rufaa
yaani makala yote Freeman Mbowe, Ester Matiko Walivyodishwa Gereani ,Baada Ya Serikali Kukata Rufaa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Freeman Mbowe, Ester Matiko Walivyodishwa Gereani ,Baada Ya Serikali Kukata Rufaa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/11/freeman-mbowe-ester-matiko.html
0 Response to "Freeman Mbowe, Ester Matiko Walivyodishwa Gereani ,Baada Ya Serikali Kukata Rufaa"
Post a Comment