title : LHRC chaendelea kupinga adhabu ya kifo, champongeza JPM kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliohukumiwa kunyongwa
kiungo : LHRC chaendelea kupinga adhabu ya kifo, champongeza JPM kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliohukumiwa kunyongwa
LHRC chaendelea kupinga adhabu ya kifo, champongeza JPM kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliohukumiwa kunyongwa
Hussein Ndubikile,
Mwambawahabari
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesema kinaendelea kupinga uwepo wa adhabu ya kifo huku kikibainisha kumpongeza Rais wa Awamu ya Tano, Dkt John Magufuli kwa kusema hadharani kuwa hatatekeleza adhabu hiyo katika kipindi chake chote na kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliokwishahukumiwa kunyongwa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Felista Mauya wakati akitoa taarifa kwa wanahabari kuhusu Maadhimisho ya 16 ya Siku ya kupinga adhabu ya Kifo Duniani inayoadhimishwa Oktoba 10 kila mwaka.
Amesema kuwa kituo hicho kimekuwa kikifanya utetetezi kuhamasisha kufutwa adhabu ya kifo kama sehemu ya kuunga mkono mpango wa ulimwengu wa kufuta adhabu hiyo duniani.
Amebainisha kuwa LHRC kinaendelea kutoa elimu kwa jamii na kuendesha progaramu za elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na kwamba tayari wameshafungua kesi ya Kikatiba namba 22 ya mwaka huu kupinga adhabu hiyo kwa kuzingatia mifano ya nchi jirani kama Kenya, Uganda na Malawi zilizofuta adahabu ya kifo.
“Maadhimisho ya mwaka huu yana dhima isemayo hali ya maisha ya waliohukumiwa kifo ikiangazia kwenye kukuza uelewa kuhusu mazingira magumu yasiyo ya kibinadamu wanaoishi watu waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa,” amesema.
Amesisitiza kuwa takwimu za Haki za Binadamu za Tanzania za mwaka jana zilizonukuliwa kuhusu adahabu ya kifo zinaonyesha watu 472 wamehukumiwa kunyongwa kati ya wanaume ni 452 wanawake 20 na kwamba katika orodha hiyo 228 wanasubiri hukumu zao kutekelezwa na 244 rufaa zao zinaendelea kusikilizwa Mahakama ya Rufaa.
Amefafanua kuwa kitendo alichokifanya Rais Magufuli hakijawahi kutokea katika historia ya nchi huku akisisitiza kituo hicho kinatambua mchango wake katika harakati za kupinga adahabu hiyo.
Katika hatua nyingine, amesema kituo hicho kina sababu za kutosha za kupinga adhabu ya kifo ikiwemo hukumu ya kifo ni adhabu ya kikatili inayotweza utu wa mtu, adhabu ya kifo haiwezi kusitishwa baada ya kutekelezwa ikiwa imetolewa kimakosa, hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba adhabu ya kifo inaweza kupunguza makosa ya jinai kuliko kifungo na kwa sasa takribani nchi 106 duniani zimefuta adhabu ya kifo.
Wakati huo huo, kituo hicho kimetoa mapendekezo kupiga hatua kuelekea kufuta adahabu hiyo ikiwemo Serikali kuwafutia adhabu wafungwa walohukumiwa vifo waliokaa magerezani muda mrefu, Serikali kuwaboreshea mazingira wafungwa waliohukumiwa kifo, kuweka rasmi tamko kutotekeleza adhabau ya kifo kulingana na maazimio ya Umoja wa Mataifa pamoja na kurekebisha sheria ya kanuni inayotoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji na uhaini kwa uwepo wa adhabu mbadala.
Pia kituo hicho kimetoa mapendekezo kwa wadau ikiwemo kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda haki ya kuishi pamoja na kuelimisha umma kuhusu mchakato unaoendelea wa mabadiliko ya katiba ili kufuta adhabu ya kifo.
Hivyo makala LHRC chaendelea kupinga adhabu ya kifo, champongeza JPM kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliohukumiwa kunyongwa
yaani makala yote LHRC chaendelea kupinga adhabu ya kifo, champongeza JPM kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliohukumiwa kunyongwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala LHRC chaendelea kupinga adhabu ya kifo, champongeza JPM kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliohukumiwa kunyongwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/lhrc-chaendelea-kupinga-adhabu-ya-kifo.html
0 Response to "LHRC chaendelea kupinga adhabu ya kifo, champongeza JPM kwa kutoa msamaha kwa wafungwa 62 waliohukumiwa kunyongwa"
Post a Comment