WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA

WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA
kiungo : WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA

soma pia


WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

WAZIRI wa ulinzi na jeshi lakujenga taifa Dr Hussein Mwinyi ameupongeza uongozi wa shule ya sekondari yaKawawa kwa ujenzi wa jengo la kisasa la utawala ambalo litachangia katika ufanisi bora wa kazi kwa walimu na wafanyakazi wote wa shule hiyo.

Akizungumza wakati wa kuzindua jingo hilo la utawala waziri Mwinyi alisema kuwa jengo limejengwa kwa viwango ambavyo serikali ya awamu ya tano inataka na jingo hilo linaviwango vinavyotakiwa.“Kwa kweli nisiwe mchoyo wa fadhila jengo hili limejengwa kwa kuzingatia ujenzi unaotakiwa na lina ramani ambayo itadumu kwa miaka mingi na itakuwa auheni kwa wafanyakazi kufanya kazi zao kwenye jengo hili” alisema Mwinyi

Waziri Mwinyi aliwataka wafanyakzi wa shule hiyo kuhakikisha wanalitunza jengo hilo pamoja na miundo mbinu yake kwa ajili ya vizazi vingine. Awali akisoma risala kwa waziri Mwinyi mkuu wa shule hiyo Meja Erenest Sikaponda alisema kuwa jengo hilo la utawala limejengwa kwa shilingi 222,591,000 na kufanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi 103,360,000 kwa kuwa hapo awali BOQ ilikuwa inaonyesha kuwa gharama za jengo ni shilingi 325,951,000.

Kupungua kwa gharama hizo ni kutokana na ubunifu,matumizi mazuri ya rasilimali,nidhamu katika matumizi ya fedha,nguvu kazi ya vijana ambao baadhi yao walikuwa mafundi na gari kubwa la kusombea mchanga,kifusi na mawe msaada huo ulitoka katika kikosi cha 841kj Mafinga” alisema Maj Sikaponda Maj Sikaponda aliwashukuru wadau mbalimbali ambao walitoa msaada wa hali na mali kusaidia ujenzi wa jengo hilo la kisasa la utawala ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa wafanyakazi wa shule hiyo.
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye jengo la utawala la shule ya sekondari Kawawa wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu wa jeshi ya JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kawawa iliyopo Mafinga Mkoani Iringa.
Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi akiwa na baadhi ya maafisa wa jeshi la JKT kikosi cha 841 KJ Mafinga pamoja na mkuu JKT Tanzania Maj Gen SM Busungu wakiwa kwenye picha ya pamoja
Na hili ndio jengo la kisasa la utawala la shule ya sekondari ya kawawa lililofunguliwa na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Hussein Mwinyi




Hivyo makala WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA

yaani makala yote WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/waziri-dr-hussein-mwinyi-azindua-jengo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI DR HUSSEIN MWINYI AZINDUA JENGO LA KISASA LA UTAWALA SHULE YA SEKONDARI KAWAWA MJINI MAFINGA"

Post a Comment