title : KUSIKILIZA KERO ZA WALIMU IMESAIDIA KUJENGA ARI YA KUFUNDISHA
kiungo : KUSIKILIZA KERO ZA WALIMU IMESAIDIA KUJENGA ARI YA KUFUNDISHA
KUSIKILIZA KERO ZA WALIMU IMESAIDIA KUJENGA ARI YA KUFUNDISHA
Na .John Luhende
Mwambawa habari
KATIKA kuwajengea uwezo wa kufundisha darasani walimu wa shule za sekonari Wilayani Ilala , Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeandaa utaratibu wa kusikiliza kero za walimu na kuzipatia majawabu ,pamoja na kuwapa mafunzo kwa vitendo ili kuboresha ufundishaji masomo ya sayansi kwa vitendo.
Hayo yamesemwa na Afisa elimu Sekondari wilaya ya ilala Elizabeth Ngonyani alipokuwa katika mkutano na walimu wa Cluster ya Kimanga uliofanyika katika shule ya secondary Tambaza na kueleza kuwa moja ya mambo yaliyokuwa yanachangia matokeo mabaya nipamoja na baadhi ya walimu hawakusoma masomo ya sayansi kwa vitendo.
“Tunao walimu mahili waliobobea katika kufundisha haondiyo watawafundisha walimu ambao hawakusoma masomo ya sayansi kwa vitendo ili nao wakafundishe wanafunzi tuligundua kuwa baadhi ya walimu walikuwa hawaelewi kufundisha kwa vitendo na wengine walikuwa wakitumia muda mwingi kufundisha shule binafsi nao tumeongea nao wameacha wanaendelea kufundisha sasa katika shule zetu” alisema
Aidha Ngonyani amesema moja ya kero za walimu ambazo zimefanyiwa kazi ni pamoja na kulipa madai yao mbalimbali na kuwapandisha madaraja baada ya kusimama kwa muda .
“Kwajumla kuu tumelipa shilingi million 246,324800 nakadritunavyo patafedha tutaendelea kuwalipa, nahapa tunaongea nawalimu kuwafahamisha mambolimbali wafahamu kwamba serikali inafanyia kazi kero zao natupo hapa watumishi wote kutoka ofisi yangu utumishi na TSD kutatua kero zao “alisema
Pamoja na hayo ametoa wito kwa walimu kufanya kazi kwa bidii ilikuongeza ufaulu katika shule za Wilaya hiyo katika mtihani wa taifa unaotarajiwa kufanyika mwezi novemba mwakahuu.
“Niwaombe walimu wa Ilala, hiikuona shule zetu zinakuwa za mwisho inatuumiza sana nawaomba wajitahidi wafundishe kilammoja amalize mtaala wake haijalishi ni kidato cha ngapi kwamaana bila kumaliza mtaala nivigumu kufaulu, naomba pia walimu wakuu wawasimamie walimu kilammoja ahakikishe ana vitendeakazi “alisema .
Kwa upande waowanafunzi ,Ngonyani amewataka kusoma kwa bidii katika sikuzilizobaki kuelekea mtihani wa taifa na waache kutegema kuiba mitihani bali wasome kinachofundishwa na walimu wao.
Hivyo makala KUSIKILIZA KERO ZA WALIMU IMESAIDIA KUJENGA ARI YA KUFUNDISHA
yaani makala yote KUSIKILIZA KERO ZA WALIMU IMESAIDIA KUJENGA ARI YA KUFUNDISHA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KUSIKILIZA KERO ZA WALIMU IMESAIDIA KUJENGA ARI YA KUFUNDISHA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/kusikiliza-kero-za-walimu-imesaidia.html
0 Response to "KUSIKILIZA KERO ZA WALIMU IMESAIDIA KUJENGA ARI YA KUFUNDISHA"
Post a Comment