title : JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU.
kiungo : JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU.
JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future unaotekelezwa katika wilaya za mkoa wa Iringa na Mbeya.
Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa hati za kimira wanawake wa kibarbaigi walisema kuwa awali walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali yoyote ile bali mali zote zilikuwa zinamilikiwa na wanaume.
“Kwenye kabila letu mila zinawapa sana nafasi wanaume kumiliki mali na vitu vingine na kumfanya wanamke kuwa tegemezi jambo ambalo miaka ya nyuma limerudisha maendeleo nyuma ya wanawake” walisema wanawake hao wa Kibarbaigi
Wanawake hao walisema kuwa baada ya kupata elimu ya upimaji wa ardhi na kuifanya ardhi kuwa na hati miliki imesaidia wanaume wa kabila hilo kuanza kuitambua nafasi ya mwanamke na kumuwezesha mwanamke naye kumiliki mali sawa na wanaume wa kabila la wabarbaigi.
Tunaishukuru serikali na mradi wa LTA kwa elimu waliyoitoa kwa wanaume wa kabila la Barbaigi kwa kukubali wanawake wamiliki ardhi kwa kupewa hati miliki za kimira bila elimu hiyo wanawake sisi tungeendelea kuwa wakina mama wa nyumbani tu.
Naye mwenyekiti wa kabila hilo la wafugaji Shabani Ntasham alisema kuwa kupatikana kwa hati miliki za kimira kumekomesha hamahama ya jamii hiyo pamoja na kumuwezesha mwanamke wa jamii hiyo kumiliki ardhi.
Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa utoaji wa hati hizo katika kijiji cha Kitisi ambapo jamii ya wabarbaigi wanaishi maeneo hayo nao walipewa hati miliki za kimira na kuanza kukomesha hama hama ya kabili hilo la wafugaji
Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wakiwa kwenye picha na viongozi mara baada ya kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future.
Hivyo makala JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU.
yaani makala yote JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/jamii-ya-wabarbaigi-wapata-hati-miliki.html
0 Response to "JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUMU."
Post a Comment