title : HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI
kiungo : HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI
HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI
Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Pwani walipotembelea hospital ya wilaya ya Bagamoyo kuadhimisha wiki ya wanawake UWT kimkoa ,(wa pili kulia ) Mganga Mfawidhi hospitalini hapo dokta Erick Mulokozi.
NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO
HOSPITAL ya wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawa, watumishi na uchakavu wa baadhi ya majengo. Akieleza changamoto hizo wakati umoja wa wanawake (UWT ) Mkoani Pwani ,ulipotembelea wodi ya wanawake hospitalini hapo, Mganga Mfawidhi wa hospital ya Bagamoyo, Dokta Erick Mulokozi alisema, tatizo la madawa limekuwa kubwa kutokana na miaka mitatu iliyopita kuwa na deni la milioni 200 walilokuwa wakidaiwa na bohari kuu ya madawa (MSD).
Alisema, walikubaliana na bohari ya dawa kwamba ikija fedha za ruzuku inakata fedha ,kulipa deni ambapo sasa wamelipunguza na kubakia na deni la sh. milioni 78. Dokta Mulokozi alieleza, fedha wanazozipata wanajiendesha kwa tozo ambayo wananunulia dawa ,kulipa posho wafanyakazi ,lakini hakuna tatizo la dawa muhimu kwa asilimia 95.
"Dawa muhimu zote zipo ,licha ya changamoto chache zilizopo na tunaendelea kupambana na hali hiyo ili kuwahudumia wananchi " alielezea dokta Mulokozi .
Kuhusiana na uchakavu wa baadhi ya majengo alisema ,hospital hiyo imejengwa mwaka 1892, hivyo yapo majengo ambayo ni lazima yawe chakavu. Akizungumzia changamoto ya upungufu wa watumishi, dokta Mulokozi alisema, imetokana na tatizo la vyeti feki, ambapo zoezi hilo lilisababisha upungufu kuzidi lakini wameshapangiwa watumishi 19, suala ambalo wanaamini itasaidia kupunguza tatizo hilo.
Nae mbunge wa viti maalum mkoani Pwani, Subira Mgalu alisema, kutokana na uhaba wa watumishi mkoa wa Pwani serikali imeshapeleka watumishi 273 wa sekta ya afya. Aliishukuru serikali chini ya Rais dk.John Magufuli kwa kutatua changamoto hiyo awamu kwa awamu. Subira alieleza, kati ya watumishi hao wilaya ya Bagamoyo wamepata watumishi 19 na Chalinze 44.
Alisema ,jitihada zinaendelea na kwamba ikitangazwa watapeleka maombi ili kuomba watumishi wanaohitajika.
Kwa upande wake ,kaimu mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani ,Arafa Kisela alisema mkoa huo, una wilaya nane za kichama na matawi 1,097 ya UWT na kata 113 .
Alifafanua ,wanaadhimisha wiki ya wanawake ya UWT ,kimkoa kwa kufanya shughuli za kijamii na kutembelea wodi ya wanawake na kujua changamoto zilizopo katika hospital ya wilaya ya Bagamoyo ,gereza la Kigongoni ,kituo cha watoto yatima na ujenzi wa kituo cha afya Yombo .
Tamko la UWT mkoa , wanakemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya madereva wa vyombo vya moto na majini kwa kusababisha vifo kwa uzembe kwani waathirika wakuu ni wanawake ,watoto na wazee.
Mbunge wa viti maalum mkoani Pwani ,Subira Mgalu alipoungana na baadhi ya viongozi wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Mkoani Pwani na wilaya ya Bagamoyo kutembelea kituo cha watoto yatima ikiwa ni moja ya shughuli walizozifanya kuadhimisha wiki ya wanawake UWT kimkoa .(Picha na Mwamvua Mwinyi)
Hivyo makala HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI
yaani makala yote HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/hospital-ya-bagamoyo-yakabiliwa-na.html
0 Response to "HOSPITAL YA BAGAMOYO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI NA BAADHI YA MAJENGO KUWA CHAKAVU - DKT. MULOKOZI"
Post a Comment