title : HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA
kiungo : HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA
HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA
Na Mathias Canal-WK, Dodoma
Serikali imeipa changamoto Bodi ya sukari nchini kutekeleza majukumu yake kwa weledi ikiwa ni pamoja na kusisitiza kuhuisha uzalishaji wa sukari kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.
KaMpuni mbalimbali za uzalishaji wa sukari nchini zimeitikia wito wa Serikali wa kuongeza uzalishaji wa sukari ili nchi iweze kujitegemea kwa bidhaa hiyo pendwa kwa matumizi ya nyumbani na viwandani na ziada jambo litalopelekea Bodi ya sukari kusimamia majukumu yake ipasavyo ili kuondokana na uagizaji wa sukari nje ya nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo jumatatu tarehe 29 Octoba 2018 na Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma.
Waziri Tizeba amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Sukari nchini Bi Mwamini Juma Malemi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi Kudhibiti sukari inayoingia nchini pasina utaratibu huku akiwataka kusimamia kwa weledi ufanisi katika uongezaji wa uzalishaji wa sukari nchini.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, Oktoba 29, 2018.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenneth Michael Kitundu Bengesi akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu tarehe 29 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akimkabidhi muongozo wa utendaji kazi Mwenyekiti wa Bodi ya sukari Tanzania Bi Mwamini Juma Malemi kwenye uzinduzi wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma, jumatatu Octoba 29,2018.
Hivyo makala HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA
yaani makala yote HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/hatuwezi-kuendelea-kuagiza-sukari.html
0 Response to "HATUWEZI KUENDELEA KUAGIZA SUKARI WAKATI TUNA UWEZO WA KUFANIKISHA UZALISHAJI-DKT TIZEBA"
Post a Comment