Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu

Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu
kiungo : Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu

soma pia


Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu

Na Teresia Mhagama, Ruvuma
Naibu Waziri wa Nishati, Subira  Mgalu, amewataka wataalam katika Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwa makini katika kazi ya upangaji wa vijiji vinavyopaswa kupelekewa umeme kwenye wilaya zenye majimbo mawili ya uchaguzi ili kuepusha malalamiko ya kupendelea upande mmoja wa Wilaya. Aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akikagua miradi ya usambazaji umeme vijijini katika Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo Wilaya hiyo ina Jimbo la Tunduru Kusini na Tunduru Kaskazini.

Naibu Waziri alitoa agizo hilo baada ya kupata malalamiko kuwa, Vijiji vingi vya Tunduru Kaskazini ndivyo vimesambaziwa umeme huku Tunduru Kusini ikiwa na Vijiji vichache. Aidha, Naibu Waziri aliagiza kuwa, kazi ya upangaji wa Vijiji vinavyotarajiwa kupelekewa umeme kupitia miradi mbalimbali ishirikishe viongozi wa ngazi mbalimbali katika maeneo ili kuondoa malalamiko katika miradi hiyo.

Vilevile alisema kuwa, wataalam hao wahakikishe kuwa hawaruki Vijiji na badala yake kila kijiji kinachopitiwa na mradi kisambaziwe nishati ya umeme. Kuhusu kazi ya uunganishaji Wilaya ya Tunduru  kwenye umeme wa gridi,  Naibu Waziri alisema kuwa, wilaya hiyo itaanza kupata  umeme huo kuanzia mwezi Machi mwakani baada ya kuvuta umeme kutokea wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi, (hawapo pichani) kabla ya kuzindua huduma ya umeme katika Kijiji cha Hanga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma. Wa kwanza kushoto ni Mbunge wa Namtumbo, Eng. Edwin Ngonyani na kushoto kwa Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Sophia Mfaume.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Mtakanini, wilayani Namtumbo mkoani  Ruvuma.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi baada ya kuwasha rasmi umeme katika Kijiji cha Mchuluka wilayani Tunduru mkoani  Ruvuma.
Baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Hanga, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakati alipofika kijijini hapo kukagua  mradi wa usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme katika Kijiji hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu

yaani makala yote Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/12/wilaya-zenye-majimbo-mawili-ziangaliwe.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wilaya zenye majimbo mawili ziangaliwe kwa umakini katika upangaji wa miradi ya umeme vijijini – Mgalu"

Post a Comment