HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA

HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA
kiungo : HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA

soma pia


HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA

Na Karama Kenyunko, globu ya jamii.

Hatimaye Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na viongizi wenzake nane wa Chadema, leo amepata wakili wa kumtetea dhidi ya kesi hiyo inayounguruma katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, 

wakili Jamuhuri Johnson amejitambulisha leo Oktoba 25.2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja leo kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH).Hatua hiyo imefikwa baada ya Wakili aliyekuwa akimtetea Msigwa, Jeremiah Mtobesya kujitoa Agosti 23, mwaka huu.

Wakili Jamuhuri amedai kulingana na umuhimu wa kesi hiyo ameomba ahirisho ili apate muda wa kupitia jalada la kesi hiyo na na pia ameomba kupatiwa mwenendo mzima wa kesi tangia ilipoanza ili aweze kumwakilisha mteja wake huyo vizuri.

Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi aliiomba mahakama kutupilia mbali maombi hayo ya wakili Jamuhuri na kudai kuwa wanapinga kwa sababu kwa kuangalia mwenendo wa kesi hiyo ni wazi katika kesi ya msingi hakuna hatua yoyote iliyopigwa zaidi ya washtakiwa kusomewa mashtaka yanayowakabili.

Katika kuwasomea washtakiwa Maelezo ya awali (PH) wahusika wakuu ni washtakiwa ambao wakisomewa ndiyo wanawajibu wa kujibu kipi wanakubali na kipi hawakikubali. Baada ya Nchimbi kueleza hayo, wakili wa Msigwa, Jonson alieleza kuwa mteja wake siyo mwanasheria kuna maelezo ambayo amempatia hayaelewi vizuri ndiyo sababu aliomba kupitia jalada.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba Mosi, mwaka huu asubuhi kwa ajili ya PH.Mbali na Msigwa washtakiwa wengine ni ambao wanatetewa na Wakili Kibatala ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, mbunge wa bunda, Esther Bulaya, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko na katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.


Hivyo makala HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA

yaani makala yote HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/hatimaye-mbunge-peter-msigwa-apata.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "HATIMAYE MBUNGE PETER MSIGWA APATA WAKILI WA KUMTETEA"

Post a Comment