Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili

Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili
kiungo : Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili

soma pia


Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili


Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa wiki mbili kwa vilabu vyote vya mchezo wa Kriketi nchini ambavyo havijasajiliwa  kufika Baraza la Michezo La Taifa kwa ajili ya kujisajili .

Akizungumza na wadau hao wa mchezo huo jana katika Ukimbi wa mikutano  uliopo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa ni wajibu wa kila kilabu cha mchezo nchini kufuata sheria na taratibu zinazosimamia sekta ya michezo.

“Kama kuna kilabu chochote cha mchezo wa kikreti kipo na hakijasajiliwa, natoa wiki mbili  kuweza kufuata taratibu na sheria za usajili ili viweze kutambulika kisheria ” alisema Dkt. Mwakyembe.

Aidha aliongeza kwa kuutaka uongozi wa Chama cha Kriketi Tanzania kuhakikisha unatenga siku moja  kwa ajili ya mkutano na wanachama wake ili kupata nafasi ya kupitia vipengele vinavyounda katiba ya chama hicho kwa ajili ya maboresho mbalimbali.

Vilevile Waziri Dkt. Mwakyembe  alipata fursa ya kusikiliza changamoto mbalimbali  zinazokikabili chama hicho cha mchezo wa Kriketi na kuhaidi kuzifanyia kazi changamoto hizo.

Kwa Upande wake Kaimu Katibu  Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw.Makoye  Nkenyenge amewataka wanachama hao kufanyia kazi maagizo yaliyotolewa na Waziri Dkt. Mwakyembe kwa kuhakikisha wanasajili vilabu vyote ambavyo havijasajiliwa.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania Bw. Taher Kitisa ameahidi kushirikiana na wanachama wenzake katika kuhakikisha wanapitia katiba ya chama hicho na kuifanyia maboresho.

Dkt. Mwakyembe alikutana na wanachama wa Kriketi  zaidi ya 60 lengo ikiwa ni kujadiliana mambo mbalimbali yanayohusu mchezo huo ikiwemo uboreshwaji wa uongozi wa chama hicho kwa manufaa  ya ustawi wa mchezo huo.


Hivyo makala Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili

yaani makala yote Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/dkt-mwakyembe-avipa-wiki-mbili-vilabu_2.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Dkt. Mwakyembe Avipa Wiki Mbili Vilabu Vya Mchezo Wa Kriketi kujisajili"

Post a Comment