Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga

Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga
kiungo : Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga

soma pia


Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga

BENKI ya NMB imetoa msaada wa mahema maalum pamoja na fulana zitakazotumiwa na Taasisi ya Suleman Kova Security and Disaster Management Foundation-Sukos-DMF wakati inazunguka kwa jamii kutoa elimu namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotekea. Vifaa hivyo ambavyo ni mahema maalum nane pamoja na fulana zitakuwa zikitumiwa siku ya tarehe 6 Octoba ikiwa ni siku maalumu kabisa ya kuadhimisha siku ya maafa /majanga duniani. 


Akizungumza katika tukio hilo la kukabidhi msaada huo, Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba alisema tukio hilo ni mwendelezo wa benki hiyo katika kuisaidia jamii hivyo wanatambua na kuguswa na majanga na maafa yanayowakumba wananchi ambao ni jamii wanaoihudumia.

"Ni ada yetu NMB kuisaidia jamii inayotuzunguka kupitia kitengo maalumu cha CSR...tumekuwa tukifanya hivi maeneo mbalimbali..hususani sekta ya elimu, afya na huduma nyingine muhimu kwa jamii. NMB inaamini msaada huu utatasidia jamii kupatiwa elimu ya kujikinga na majanga unaweza kupunguza athari ya majanga hayo hata yanapotokea," alisema Bi. Lilian Kisamba alipokuwa akikabidhi msaada huo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Sukos-DMF, Suleiman Kova.

Alisema NMB itaendelea kuisaidia jamii katika maeneo mbalimbali kwa kuwa hakuna maendeleo ya kiuchumi pasipo na jamii salama na pia hakuna biashara inayoweza kufanya vema pasipo na jamii salama. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Sukos-DMF, Suleiman Kova (Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi) alisema taasisi yake ya Sukos-DMF kwa kushirikiana na Benki ya NMB na wadau wengine imepanga kufanya uzinduzi wa mahema maalum ambayo yatakuwa yakitumika katika shughuli za kutoa hifadhi kwa wahanga wakati yanapotokea maafa.

Alisema zoezi hilo litakwenda sambamba na washiriki kufanya mazoezi (jogging) kuanzia eneo la uwanja wa taifa kuelekea viwanja vya Kituo cha Vijana cha Jakaya Kikwete na pia kutakuwa na tukio la washiriki kuchangia damu kwa ajili ya wahitaji, huku akisisitiza elimu ya kukabiliana na majanga kwa taasisi hiyo utakuwa ni mradi endelevu.

Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba (wa pili kuklia) akizungumza na wanahabari kabla ya kukabidhi mahema nane ambayo yatolewa na NMB ambayo yatatumiwa na taasisi hiyo wakati inazunguka kwa jamii kutoa elimu namna ya kukabiliana na majanga mbalimbali pindi yanapotekea.
Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Suleman Kova Security and Disaster Management Foundation, Sukos-DMF, Bw. Suleiman Kova (Kamanda mstaafu wa Jeshi la Polisi) moja ya fulana zilizotolewa na NMB kwa ajili ya Sukos-DMF. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Suleman Kova Security and Disaster Management Foundation, Sukos-DMF, Bw. Suleiman Kova (wa pili kulia) akizungumzia taasisi yake inavyofanya kazi zake kabla ya kupokeaa msaada huo toka NMB. Kutoka kushoto ni Msanii wa uigizaji, Salim Ahmad 'Gabo', Meneja Mwajiri wa Cops Security (T) Ltd, Ibraahim Mcherecheta na Meneja Mradi, Uwajibikaji kwa Jamii wa Benki ya NMB, Lilian Kisamba (wa kwanza  kulia). 



Hivyo makala Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga

yaani makala yote Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/benki-ya-nmb-yaisaidia-sukos-dmf-vifaa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Benki ya NMB yaisaidia sukos, dmf vifaa vya kukabiliana na maafa /majanga"

Post a Comment