Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro

Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro
kiungo : Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro

soma pia


Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro

Benki ya Biashara Mkombozi imezindua rasmi Tawi la Morogoro ambalo limepandishwa hadhi kutoka kituo cha huduma za kifedha na sasa kuwa tawi kamili.

Zoezi hili linafanyika wiki moja tu baada ya Benki ya Biashara Mkombozi kuzindua Tawi la Tegeta ambalo pia lilikuwa kituo cha cha huduma za kifedha hapo awali.

 Ufunguzi wa Tawi hilo ulifanywa na Katibu Tawala Wilaya ya Morogoro Bi. Ruth John akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa,  wadau mbalimbali, wafanyakazi, wafanyabiashara na wateja wa Benki ya Biashara Mkombozi.

 Akizindua tawi hilo jipya, mgeni rasmi aliipongeza Benki ya Biashara Mkombozi kwa hatua iliyofikia na kusema uzoefu kutoka nchi nyingine unaonyesha kuwa wafanya biashara wadogo na wale wakati ni wadau muhimu sana katika kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

“Hivyo napenda kuwapongeza benki ya Biashara Mkombozi kwa kuamua kuwafikia wadau hawa muhimu ambao baadhi ya taasisi za kifedha zinawatizama kama ni soko hatarishi katika biashara ya kukopesha,” alisema.

Mgeni rasmi pia aliipongeza Benki ya Biashara Mkombozi kwa kutoa huduma za kibenki kwa watanzania wote bila ubaguzi wa rangi, ukabila, dini, dhehebu tofauti na baadhi ya watu wanavyotafsiri kuwa ni benki ya kanisa tu.

 “Natambua kuwa bado tuna changamoto kubwa ya kuwafikia na kuwashawishi watanzania walio wengi kutumia huduma za fedha za kibenki. Rai yangu kwenu Uongozi na Wafanyakazi wa Benki ya Biashara Mkombozi ni kwamba, mjikite zaidi katika ubunifu ili kuweza kuwavutia kundi hili ambalo linahitaji huduma zenu lakini labda utambuzi bayana bado haujakuwepo,” alisema.

Alitoa wito kwa Benki ya Mkombozi pia ijitahidi kufahamu mahitaji halisi ya soko na hivyo kuboresha huduma zake na bidhaa ili ziendane na mahitaji. “Elimu juu ya fedha kwa wananchi (yaani Financial literacy) ni muhimu sana, naomba pia muweke nguvu zenu katika hili,” alisema.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John  (wa tatu kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tawi jipya la Morogoro la Benki ya Biashara ya Mkombozi  huku viongozi na wageni waalikwa wakishuhudia tukio hilo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro, Ruth John akijaza fomu ya kufungua akaunti katika Benki ya Biashara ya Mkombozi baada ya kuzindua tawi jipya la Morogoro. 

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Biashara ya Mkombozi Tawi la Morogoro wakifuatilia matukio ya uzinduzi wa tawi hilo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro

yaani makala yote Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/benki-ya-biashara-ya-mkombozi-yazindua_20.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Benki ya Biashara ya Mkombozi yazindua Tawi la Morogoro"

Post a Comment