title : ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU
kiungo : ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU
ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU
Serikali imesema Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 imeweka masharti kwa mashirika yaliyokuwa yamesajiliwa katika Sheria nyingine na yanasifa za kusajiliwa kama Mashirika Yasiyo ya Kiserikali, kuomba Cheti cha Ukubalifu chini ya Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Hayo yamesema mapema leo mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya usimamizi wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii.
Waziri Ummy Mwalimu amesema kimsingi Cheti cha Ukubalifu kinatolewa ili kuyaweka Mashirika yote Yasiyo ya Kiserikali chini ya usimamizi mmoja ili kuondokana na changamoto za awali ambapo mashirika hayo yalikuwa yakiratibiwa chini ya Sheria na Mamlaka zaidi ya moja.
Waziri Ummy aliwaambia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa kutokana na kutungwa kwa Sera na Sheria hii kwa mara ya kwanza Tafsiri ya “Shirika Lisilo la Kiserikali” ilipatikana rasmi akiongeza kuwa Tafsiri hii inayotofautisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Asasi nyingine za kiraia kama vile Jumuia za kijamii zinazosajili Wizara ya Mambo ya Ndani, Makampuni yanayosajiliwa BRELA na Bodi za wadhamini zinazosajiliwa na RITA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akitoa taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma kushoto ni Niabu wake Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitoa maelezo kuhusu usimamizi wa uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kusaidia makundi maalum nchini wakati Wizara ilipokuwa ikiwasilisha taarifa kuhusu usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo jijini Dodoma kushoto ni Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba akitoa maoni yake kwa Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto walipowasilisha taarifa ya usimamizi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mbele ya Kamati yake jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. John Jingu akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo jijini Dodoma kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na itakavyosaidia kuweka uwazi na uwajibikaji kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile.
Hivyo makala ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU
yaani makala yote ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/ashirika-yenye-sifa-kama-za-ngos.html
0 Response to "ASHIRIKA YENYE SIFA KAMA ZA NGOs YATAKIWA KUWA NA CHETI CHA UKUBALIFU"
Post a Comment