title : WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI
kiungo : WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI
WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amewataka wananchi kupata taarifa sahii kutoka wizara yake na kuacha mara moja kutumia mitandao ya kijamii vibaya na kupotosha jamii.
Ameyasema hayo leo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kampeni ya umezeshaji wa dawa za kingatiba dhidi ya Kichocho na Minyoo ya tumbo nchini.Amesema waathirika wakubwa wa Kichocho na Minyoo ya tumbo ni watoto wenye umri wa kwenda shule,yaani watoto wenye umri kati ya miaka 5 na 14 ambao wanakuwa katika shule za msingi.
“Tunachotoa ni KINGATIBA na sio Chanjo,dawa hizi ni salama na zimethibitishwa ubora wake na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) pamoja na Shirika la Afya Duniani(WHO) pia zimesajiliwa kulingana na taratibu za nchi na mamlaka husika.
Amesema dawa hizo huimarisha afya ya mtoto na hivyo kujenga taifa lenye afya bora,nguvu ya kutosha ili kuleta maendeleo.
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akisisitiza jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na sintofahamu iliyozuka miongoni mwa jamii kuhusu utumiaji wa dawa kinga za minyoo na kichocho jijini Dodoma.
Naibu waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Mh. Faustine Ndugulile akisisitiza jambo juu ya matumizi ya dawa kinga za minyoo na kichocho ambazo zinatolewa hivi sasa katika jamii na kuwatoa hofu wananchi juu ya dhana potofu kuwa dawa hizo zina madhara.
Baadhi ya waandishi wa habari wakipata dawa kinga za minyoo na kichocho kutoka kwa Meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele nchini (NTD) Dkt. Upendo Mwingira baada ya kikao kilichomuhusisha Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto na waandishi wa habari kuzungumzia dhana potofu iliyotanda katika jamii kuhusiana na madhara ya dawa hizo.
Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akionesha dawa kinga za minyoo na kichocho zinazotolewa katika jamii hivi sasa na kuwataka wananchi wasihofu kumeza dawa hizo ambazo hazina madhara yeyote kiafya, wakati akifanya mahojiano ya moja kwa moja na kituo cha ITV.
Hivyo makala WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI
yaani makala yote WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waziri-ummy-atoa-ufafanuzi-kuhusu.html
0 Response to "WAZIRI UMMY ATOA UFAFANUZI KUHUSU KAMPENI YA UMEZESHAJI WA DAWA ZA KINGATIBA DHIDI YA KICHOCHO NA MINYOO YA TUMBO NCHINI"
Post a Comment