WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA

WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA
kiungo : WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA

soma pia


WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatakaWatanzania waishio nje ya nchi wahakikishe wanashiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao kwa kushawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa waje kuwekeza nchini na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais, Dkt. John Magufuli inaamini kuwa Tanzania itapata maendeleo makubwa ya kiuchumi endapo wananchi wake watatekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya “Hapa Kazi tu”.

Aliyasema hayo jana jioni (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakatiakizungumza na Watanzania waishio nchini China kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzani uliopo jijini Beijing. 

Alisema nchi zote zilizoendelea zilihakikisha kuwa wananchi wake wanaelewa na kutekeleza matamko yanayowahamasisha kufanya kazi, hivyo alitumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania popote walipo kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu.’

Waziri Mkuu alisema China ambayo imefanikiwa kuwa moja kati ya nchi zenye nguvu kubwa ya kiuchumi duniani, imefika hapo kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na wananchi wake, ambao waliamua kuunga mkono juhudi za Serikali yao kwa kufanya kazi kwa bidii na weledi wakiwa ndani au nje ya nchi. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nje ya nchi wajiepushe na vitendo vya uhalifu hasa biashara ya dawa za kulevya ambayo inachafua jina na heshima ya nchi yao kimataifa. “Tanzania ni nchi nzuri na inaheshimika duniani, nawasihi wote mnaoishi nje muachane kabisa na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa sababu inalitia doa Taifa na adhabu yake katika baadhi ya nchi ni kifo,” alisisitiza Waziri Mkuu.

Awali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga alisema mwelekeo wa Diplomasia ya Tanzania Kimataifa hivi sasa ni kiuchumi (economic diplomacy), hivyo Watanzania waishio nje wanapaswa kuwa wabunifu, makini katika kutafuta fursa zenye manufaa kwa nchi yao.

Alisema Diplomasia ya Uchimi si kupeleka Tanzania wawekezaji tu bali wawekezaji katika viwanda ambavyo kila vinapojengwa vinachangia kuinua uchumi wa Taifa.Kwa upande wake,Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki aliwaasa vijana kuitumia teknolojia ya mawasiliano na mitando ya jamii kutafuta habari na taarifa muhimu hasa nafasi za masomo ili kujiendeleza kielimu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 03, 2018.


Hivyo makala WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA

yaani makala yote WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/watanzania-waishio-nje-watakiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WATANZANIA WAISHIO NJE WATAKIWA KUSHAWISHI WAWEKEZAJI-MAJALIWA"

Post a Comment