title : Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF
kiungo : Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF
Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF
Jumla ya waendesha bodaboda 117 kutoka wilaya ya Temeke wamejiandikisha katika mfumo wa hiari wa kuchangia mafao kwenye Shirika la Tiafa la hifadhi ya Jamii NSSF.
Hatua hii ni alama njema kwa wananchi kuendelea kutambua na kuona muhimu wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini jambo ambalo litasaidia wananchi kuweza kujiwekea akiba yao ya maisha ya baadae.
Afisa mwandamizi uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)Abbas Cothema akizungumza na waendesha bodaboda wa wilaya ya Temke ambapo amesema wameitikia wito kwa wingi wa kujiandikisha na kujichangia wenyewe kwa hiari kwamba hivyo hii ni hatua kubwa wananchi kuelewa elimu kuhusiana na suala la hifadhi zao za baade.
Cothema amesema kuwa wanachama hao wapya wataweza kufaidika na mafao mbalimbali yakiwemo mafao ya matibabu ambapo mwananchama anapata matibabu ya bure kutokana na michango yake anayoichangia kwa kila mwezi ambapo atachangia kiwango cha kuanzia kiasi cha shilingi elfu ishirini.
‘Hii ni fursa pekee kwa wananchi ambao wapo kwenye sekta isiyorasmi kuweza kujiandikisha na kujiwekea akiba ambayo itawasaidia hivyo ni wakati wao sasa nao kufaidika na matunda ya jasho lao kwa kujichangia wenyewe” alisema Cothema.
Cothema amesema mpaka sasa wameshatoa elimu kwa mikoa zaidi ya kumi ambapo wananchi wameweza kuelimishwa umuhimu wa mifuko ya hifadhi ya jamii na umuhimu wake.
NSSF imepewa jukumu la kuandikisha wanachama wapya watakaojichangia kwa hiari wenyewe.
Afisa matekelezo wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Abbas Cothema akitoa maelekezo kwa waendesha bodaboda wa wilaya ya Temeke wakati walipokuwa wakijiandikishai ili kujiunga kwenye mfumo wa Hiari wa NSSF katika kampeni ya Zamu yako maalumu kwa wananchi ambao wako kwenye sekta isiyorasmi.
Baadhi ya waendesha bodaboda wakiwa kwenye foleni ya kujiandikisha kwenye mfumo wa hiari wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF jana wilayani TemekeJijini Dar es salaam.
Afisa matekelezo Kassim Mfundo akiwaandikisha wanachama wapya kwenye mfumo wa Hiari hapo jana wilayani Temeke ambapo waendesha bodaboda 117 walijiandikisha.
Hivyo makala Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF
yaani makala yote Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/waendesha-bodaboda-117-wilaya-ya-temeke.html
0 Response to "Waendesha bodaboda 117 wilaya ya Temeke wajiunga kwa hiari NSSF"
Post a Comment