title : VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO
kiungo : VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO
VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
MAMLAKA ya Elimu na Ufundi Stadi Kanda ya Dar es Salaam imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani zaidi ya sh.milioni 41 katika Chuo cha Ufundi Maalumu Yombo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga amesema kuwa vifaa hivyo vimekwenda kwa watu muhimu katika kuwaandalia maisha ya baadaye kwa vijana wenye ulemavy mbalimbali.
Amesema kuwa msaada huo sio mwisho kutokana na mahitaji ya Chuo hicho kutoa elimu kwa vijana wenye mahitaji maalum kwani serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda ambapo vijana wanaweza kuunda vikundi na kuanzisha viwanda na kuweza kujipatia kipato na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Dkt Mwesiga amesema vifaa hivyo lazima vitumike kwa malengo ualiyokusudia ikiwa ni kujifunzia wanafunzi hao na kupata ujuzi wanaohitaji pamoja na kanda ya VETA kufatilia vifaa hivyo na maendeleo ya wanafunzi katika Chuo cha Yombo.
“Nia ya serikali ni kuona watu wenye mahitaji maalumu wanapata ujuzi kutokana na ulemavu wao na hakuna kuachwa nyuma jamii hiyo na wala kubaguliwa kwa kuwakosesha elimu”amesema Dkt. Mwesiga.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam Florence Kapinga amesema kuwa maombi ya Chuo cha Yombo yalikuwa yanamkosesha usingizi kwa kutambua vijana waliopo wana mahitaji maalum ikilinganishwa na maombi mengine.
Amesema vifaa hivyo ni katika fani Tano ambazo ni Umeme, Ushonaji, Uchongaji na Uungaji vyuma, Kilimo pamoja na Ujenzi.
Amesema kuwa vifaa vilivyokuwa vinahitajika vinatofautiana na vile vya watu wasiye na ulemavu hivyo na kufanya kupata ugumu wa uagizaji lakini nguvu ilitumika mpaka vikapatikana.
Picha ya Pamoja Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga pamoja Kanda ya VETA Dar es Salaam,Watumishi wa Chuo pamoja na wanfaunzi.
Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga akizungumza wakati hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika Chuo cha Ufundi Maalum Yombo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Maalum Yombo, Mariam Chilangwa akitoa historia fupi ya chuo hicho katika hafla iliyofanyika Chuoni hapo o jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Dkt. Patricia Mwesiga akikabidhi moja kifaa cha msaada kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufiundi Maalum Yombo, Mariam Chilangwa katika hafla iliyofanyika Chuo hapo , jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO
yaani makala yote VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/veta-kanda-ya-dar-es-salaam-yatoa.html
0 Response to "VETA KANDA YA DAR ES SALAAM YATOA MSAADA WA VIFAA CHUO CHA UFUNDI MAALUM YOMBO"
Post a Comment