title : UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO
kiungo : UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO
UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO
Balozi Seif akionyesha mshangao wake kutokana na baadhi ya Mashine nzima kutofanya kazi kutokana na ukosefu wa Wahandisi wa kuziendesha kwa sababu za kustaafu na wengine kufariki Dunia.
Kaimu Mkuu wa Karakana ya Serikali Ndugu Yussuf Kulia Masururu akimkaguza sehemu mbali mbali balozi Seif kujionea hali halisi ya Mazingira ya Karakana hiyo. Wa kwanza kutoka Kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Mihayo Juma N’hunga.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akiangalia baadhi ya vitengo vya Karakana Kuu ya Serikali iliyopo Chumbuni alipofanya ziara ya ghafla kwenye Taasisi hiyo ya Uhandisi.Aliyepo Kulia ni Kaimu Mkuu wa Karakana ya Serikali Ndugu Yussuf Masururu na nyuma ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Mh. Mohamed Ahmed Salum.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameukumbusha Uongozi wa Karakana Kuu ya Serikali kuandaa mapendekezo yatakayotoa mwanga wa kuifufua Karakana hiyo ili itoe huduma imara zilizokusudiwa kutokana na uwepo wa azma ya kujengwa kwake.
Alisema mapendekezo hayo ambayo tayari alikwisha yaagiza kwa Uongozi huo kufuatia ziara yake aliyoifanya kwenye Karakana hiyo karibu Miaka Mitano iliyopita ni vyema yakaainisha vyema mpango Mkuu wa muda mfupi wa kati na mrefu.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kumbusho hilo wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Karakana hiyo iliyopo Chumbuni kuangalia uhalisia wa mazingira halisi ya uwajibikaji wa Watendaji wake na changamoto zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi wa kila siku.
Hivyo makala UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO
yaani makala yote UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/uongozi-wa-karakana-ya-serikali-waaswa.html
0 Response to "UONGOZI WA KARAKANA YA SERIKALI WAASWA KUANDAA MAPENDEKEZO"
Post a Comment