TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro.

TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro.
kiungo : TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro.

soma pia


TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro.







Na Veronica Kazimoto -Kilimanjaro,21 Septemba, 2018                                   Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaendelea kutoa elimu ya maadili na namna bora ya kuhudumia wateja kwa watumishi wake nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo watumishi hao na kuwaongezea weledi katika majukumu yao ya kila siku.

Akiwasilisha mada kuhusu Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania katika ofisi ya TRA Moshi mkoani Kilimanjaro, Afisa Maadili Mwandamizi wa mamlaka hiyo Adelaida Rweikiza amesema kuwa  ni wajibu wa watumishi wote wa TRA kuwahudumia wateja kwa usawa na kwa kiwango cha hali ya juu.

"Ni wajibu wetu sisi watumishi wa TRA kuhakikisha tunatoa huduma bora pamoja na kutumia lugha nzuri kila tunapowahudumia wateja wetu," alisema Rwikiza.

Rweikiza ameongeza kuwa, maadili katika Utumishi wa Umma  ni jambo la msingi hivyo amewasisitiza watumishi hao kuwa waadilifu na kuepuka vitendo vya rushwa na mienendo mibaya ambayo inaweza kuharibu taswira ya TRA.

Naye, mmoja wa watumishi hao ambaye ni Afisa wa Kodi Robert Mlay amefurahishwa na kitendo cha Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoa elimu kwa watumishi wake na kufafanua kuwa, elimu hiyo itawasaidia katika kuongeza ufanisi na kutimiza malengo ya mamlaka.

"Nimejisikia vizuri sana kupata elimu hii ya maadili na namna bora ya kuwahudumia wateja kwasababu itatusaidia sisi kama watumishi wa TRA kutoa huduma kwa haki bila upendeleo wowote," alieleza Mlay.

Kwa upande wake Afisa Kodi Mwandamizi ambaye pia ni mtumishi aliyepata elimu hiyo Gloria Ngowi, ameeleza kuwa ni muhimu elimu ya maadili ifundishwe kwenye vyuo vyote 
ili vijana wanapoajiriwa katika taasisi mbalimbali waweze kufanya kazi zao kwa kufuata misingi ya maadili.

"Ninaiomba mamlaka iendelee kutoa elimu hii kwa ajili ya kutukumbusha wajibu wetu mahali pa kazi lakini pia kuna umuhimu wa vyuo vyetu nchini kufundisha somo la maadili 
kwa lengo la kuwawezesha vijana wetu kufuata misingi ya maadili kila wanapotimiza majukumu yao", alifafanua Ngowi.


Elimu ya Maadili na namna bora ya kuhudumia wateja inaendelea kutolewa kwa watumishi mbalimbali wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati elimu ya Msamaha wa Riba na Adhabu kwenye Malimbikizo ya Madeni ya Kodi na Mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018 ikitolewa kwa wafanyabiashara.


Hivyo makala TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro.

yaani makala yote TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/09/tra-yaendelea-kutowa-mafunzo-kwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TRA Yaendelea Kutowa Mafunzo Kwa Watumishi Wake Mkoani Kilimanjaro."

Post a Comment