title : RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU
kiungo : RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU
RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo (pichani) ambaye amepata ajali ya gari juzi mkoani Manyara bado amelezwa Hospitali ya Mount Meru akiendelea kupatiwa matibabu.
Akizungumza leo kwa njia ya simu na Michuzi Blogu, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Yusuf Ilembo amesema licha ya kuwa bado Kamanda Mkumbo amelezwa hospitalini hapo hali yake inaendelea vizuri.
"Bado amelezwa Hospitali ya Mount Meru akiendelea na matibabu lakini hali yake inaendelea vizuri tu,"amesema Ilembo na kuongeza msaidizi wa Kamanda Mkumbo na dereva wake ambao nao walipata ajali hiyo walisharuhusiwa na sasa wapo nyumbani.
Juzi Ilembo alipokuwa anazungumzia ajali hiyo, alisema ilitokana na kupasuka kwa gurudumu la nyuma upande wa kushoto na kusababisha gari kupinduka.
Baada ya gari kupinduka Kamanda Mkumbo aliumia kidole cha shahada na hivyo kupelekwa hospitalini kwa matibabu.Ndani ya gari hiyo pia alikuwa na msaidizi wake na dereva.
Hivyo makala RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU
yaani makala yote RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/rpc-arusha-bado-aendelea-kupatiwa.html
0 Response to "RPC ARUSHA BADO AENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA MOUNT MERU"
Post a Comment